MUME wa mwimbaji Flora Mbasha, Emmanuel
Mbasha (32), amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar
es Salaam akikabiliwa na mashitaka mawili ikiwemo ya ubakaji.
Mshtakiwa huyo ambaye ni mfanyabiashara na mwimbaji alisomewa mashitaka yake mbele ya Hakimu Mkazi, Wilberforce Luago.
Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga
alidai kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo mawili maeneo ya Tabata
Kimanga, jijini Dar es Salaam.
Katuga alidai katika shitaka la kwanza
kuwa, Mei 23, mwaka huu eneo la Tabata Kimanga, Wilaya ya Ilala, jijini
Dar es Salaam, kinyume cha sheria huku akijua ni kosa alimuingilia kwa
nguvu msichana anayedaiwa kuwa shemeji yake (jina limehifadhiwa).
Katika shitaka la pili, ilidaiwa kuwa
Mei 25, mwaka huu eneo la Tabata Kimanga, jijini Dar es Salaam, kinyume
cha sheria, mshtakiwa aliumuingilia kwa nguvu mfanyakazi wake (jina
limehifadhiwa).
Hata hivyo, mshtakiwa alikana mashitaka hayo.
Upande wa Jamhuri ulidai kuwa hauna pingamizi la dhamana.
Upande wa Jamhuri ulidai kuwa hauna pingamizi la dhamana.
Hakimu Luago alitaja masharti ya dhamana
kwa mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili, mmoja awe mtumishi wa serikali
na mwingine kutoka taasisi inayotambulika watakaosaini hati ya dhamana
ya Sh. milioni tano.
Mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti ya dhamana hivyo alipelekwa rumande na kesi iliahirishwa
hadi Juni 19, mwaka huu itakapotajwa.
hadi Juni 19, mwaka huu itakapotajwa.
Mbasha akiwa chini ya ulinzi wa askari
polisi alisindikizwa katika basi la Jeshi la Magereza kwa ajili ya
kwenda kuanza maisha mapya mahabusu ya Keko, jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment