Je wewe ni mtu wa kupenda ghafla, yaani mwanaume anapokutamkia kwamba
anakupenda huwa
unamuamini kwa kiasi gani, unakuwa ni mwepesi wa kumuamini na kujitoa kwa ajili yake au unakuwa na kujivuta vuta ili kujiridhisha kabla ya kuingia katika uhusiano? Hebu fikiri kabla ya kuamua, jipe muda kwani hakuna jambo lililo jema kama subira linapokuja swala la kupenda. Subira itakuepusha kupoteza muda wako katika mahusiano ambayo hayana mashiko wakati dhamira yako ilikuwa ni kumpata mwenzi mwenye sifa muafaka, pale utakapoingia mahali ambapo sipo. Kwa kawaida kutoka katika uhusiano huo kuna gharama kubwa na kunaweza kukusababishia matatizo mengi yakiwemo ya kiafya.
unamuamini kwa kiasi gani, unakuwa ni mwepesi wa kumuamini na kujitoa kwa ajili yake au unakuwa na kujivuta vuta ili kujiridhisha kabla ya kuingia katika uhusiano? Hebu fikiri kabla ya kuamua, jipe muda kwani hakuna jambo lililo jema kama subira linapokuja swala la kupenda. Subira itakuepusha kupoteza muda wako katika mahusiano ambayo hayana mashiko wakati dhamira yako ilikuwa ni kumpata mwenzi mwenye sifa muafaka, pale utakapoingia mahali ambapo sipo. Kwa kawaida kutoka katika uhusiano huo kuna gharama kubwa na kunaweza kukusababishia matatizo mengi yakiwemo ya kiafya.
Hapa chini nitajaribu kueleza makosa kadhaa ambayo wanayafanya wanawake linapokuja swal la kupenda:
1.Kumbadili mtu awe vile utakavyo:
Usije ukajidanganya kwamba unaweza kumbadilisha mtu mzima na akili zake.
Kama umepata mwanaume ambaye kwa mtazamo wako unamuona ana sifa muafaka
lakini anatabia ambazo huzipendi kwa mfano ulevi au kuvuta sigara vitu
ambavyo vinakukera sana, usije ukajidanganya kwamba unaweza kumbadilisha
na akaacha tabia hizo, anaweza kuacha kwa muda tu ili kukuvuta ukiingia
kingi imekula kwako, tabia hiyo inaweza kujirudia. Ni vyema kama kuna
tabia ambazo umezipenda lakini zipo ambazo huzipendi kutoka kwa mwenzi
wako, basi weka uzingativu kwenye zile tabia unazozipendfa na zile
usizozipenda achana nazo, kama ataamua mwenyewe kuziacha sawa lakini
kama akiamua kuendelea nazo, basi zisikuumize kwani unaweza kujikuta
ndoa yako inakuwa na migogoro isiyokwisha kwa sababu ya kuonekana una
ghubu kwa kujaribu kumbadilisha mwenzi wako na mwisho wake upendo
unakuwa haupo na kisirani katika ndoa kinaongezeka. Kitendo cha
kuonekana kuwa na ghubu kinaweza kumuingiza mwanaume katika tabia
nyingine mbaya ya kutotumia muda mwingi kukaa nyumbani kwake na kutafuta
kampani nyingine, kama akipata kampani ambayo siyo nzuri anaweza
kuangikia katika nyumba ndogo ambayo itamkubali bila masharti.
2.Njoo tuishi:
Unaweza kukutana na mwanaume ambaye ana nyumba nzuri au amepanga nyumba
nzuri na ana kila kitu ndani pamoja na usafiri, anakuwa mwepesi kukupa
funguo za nyumba yake ili uhamie muishi pamoja, lakini haweki msimamo
wake wazi kwamba ana matarajio gani na wewe. Kabla ya kukubali kupokea
funguo na kuhamia kwake jiulize kama unampenda kwa dhati au umekubali
kwa sababu ya nyumba yake nzuri. Kumbuka nyumba na vitu vingine
vinavyotizamika kwa macho (material things) havina mashiko linapokuja
swala la kupenda. Kupenda kunahusisha vitu vya ndani kama vile kupenda
kwa dhati bila masharti wala kuangalia sifa za nje, kuwa na amani moyoni
kila umwonapo mpenzi wako, kuwa na furaha wakati wote mnapokuwa pamoja,
kupatwa na msisimko wa mapenzi kila umwonapo au usikiapo sauti yake nk.
Lakini kama utamkubali mwanaume kirahisi kwa sababu tu kakukabidhi
funguo za nyumba yake wakati huna mapenzi ya dhati ni janga kubwa kwa
sababu hivi vitu vya nje vinaweza kutoweka kirahisi, sasa je ikitokea si
mapenzi nayo yatakuwa yamekwisha? Kumbuka kwamba kile kilichokupeleka
kwake hakipo.
3.Amekuwa ni liwazo kwako
Liwazo linaweza kuwa sehemu ya mapenzi lakini hivi vitu haviendi pamoja.
Unaweza kuwa na mwanaume ambaye mnapendana na mnakamilishana hii ni
tofauti na mwanaume unayempenda na ukamgeuza kuwa liwazo pale unapohisi
upweke. Jiulize, je ni kwamba mnapendana na mnafurahi kuwa pamoja au
unampenda kiasi kwamba huwezi kuishi bila uwepo wake. Hapa nazungumzia
utegemezi wa kihisia, yaani unakuwa king’ang’anizi mpaka mwanaume
anakuona kero, badala ya kufurahia mahusiano yenu mwanaume anakuona kuwa
ni kero kutokana na kuwa tegemezi wa kihisia. Hakuna mwanaume
anayependa mahusiano ya aina hii anachoka haraka kihisia na atajitahidi
kwa kila namna kukukwepa na ikiwezekana kukutosa na kutafuta ustaarabu
mwingine jambo ambalo litakuumiza sana.
4.Mwanaume king’ang’anizi:
Mwanaume kutongoza na kukataliwa siyo jambo linalowashughulisha sana
kwao kujaribu na kukosa ni sehemu ya maisha, lakini lipo suala la
kung’ang’ania, yaani mwanaume kumfuatilia mwanamke kwa hali na mali na
kujitoa ili kuhakikisha anampata mwanamke anayemtaka. Huu ni mtego wa
mapenzi, kwani kwa mwanaume kung’ang’ania na kufuatilia mwanamke kwa
muda mrefu bila kuchoka hata asumbuliwe kiasi gani haimaanishi kwamba
mwanaume huyo amempenda mwanamke huyo. Wakati mwingine ni matamanio tu
ndiyo yamemsukuma kutokana na sifa za nje alizo nazo mwanamke huyo.
Kupenda kwa mwanaume kunahusisha zaidi sifa za nje kuliko za ndani na
ndiyo maana mapenzi ya aina hiyo hayadumu yanaanza kama kichaa na
kuyeyuka ghafla kama kipande cha barafu juani. Pale mwanamke anapokutana
na mwanaume king’ang’anizi na asiyekubali jibu la hapana, kabla ya
kukubali ajiulize kama anakubali kuwa na mahusiano na mwanaume huyo kwa
sababu amempenda kwa dhati au kwa sababu ya uking’anga’nizi wake?
Kumbuka kwamba wapo baadhi ya wanawake wanaweza kumkubali mwanaume tu
kwa sababu amemfuatilia sana, anajiwa na huruma anakubali kuwa na
mausiano naye siyo kwa sababu amempenda bali kwa sababu ya huruma. Ni
vyema ukajiuliza kama na yeye atathamini huruma yako au akishapata
alichokitaka atakugeuka na kuwa mwiba mchungu kwako? Tafakari na chukua
hatua.
5.Baada ya kupanda mbegu mmea ukachipua
Umekuwa na uhusiano na mwanaume huyu kwa muda mrefu, lakini hakuwahi
kukutamkia kwamba ana matarajio gani na wewe kuhusiana na swala la ndao,
ghafla unakoma kuziona siku zako… Mimba hiyo! Je unafanyaje?
Kwanza naomba ufahamu kwamba, kupata mimba haimaanishi ndiyo kuolewa.
Hili ni kosa ambalo wanalifanya wanawake wengi tena wa kiwango cha
kutosha, wanaamini kwamba kubeba mimba kutawahakikishia kuolewa na
mwanaume aliyempa ujauzito. Kwa huku kwetu sheria haziwabani sana
wanaume linapokuja swal la kulea mimba na matunzo ya mtoto kwa hiyo
mwanaume kumtosa mwanamke aliyebeba ujauzito siyo jambo la kushangaza.
Wanawake ambao ni single mother wanajua kuhusu jambo hilo. Kwa hiyo kama
unabeba mimba fanya hivyo ukiwa umejiandaa kujitwika changamoto
zitakazojitokeza na usije ukajifariji ukidhani kutakuwa na masaada
kutoka kwa mwenzi wako, utakuwa unajidanganya. Kama akikubali mfunge
ndoa sawa, kama akikubali kulea mimba na mtoto atakeyezaliwa pia ni
sawa, akikataa wala usivunjike moyo, simama imara na songa mbele na
maisha kwani kuzaa kabla ya ndao siyo mwisho wa maisha, yapo maisha tena
mazuri sana ukiwa na mwanao. Kwanza unaye mtu wa kukuliwaza, na pili
utakuwa umajihakikishia kwamba wewe si mgumba, na tatu leo na kesho
umekuwa mtu mzima unaye wa kukushika bega kuliko kutegemea ndugu zako.
6.Pesa inapokuwa sehemu katika kupenda.
Wapo baadhi ya wanawake kabla ya kumkubalia mwanaume wanaangalia
anamiliki kitu gani, amesoma kwa kiwango gani, ana kazi ya aina gani,
anafanya shughuli gani, anazo fedha za kutosha au yuko katika mazingira
ya utafutaji yanayoashiria neema huko mbeleni. Sikatai kwamba wanawake
kabla ya kumkubali mwanaume wanataka kujihakikishia usalama, na kama
nilivyowahi kusema hapa mara nyingi kwamba usalama kwa mwanamke maana
yake ni mtu kuwa na fedha, tofauti na zama za kale za mawe ambapo
uwindaji na kilimo kilimuweka mwanaume shupavu katika nyanja hizo
kukimbiliwa na wanawake. Siku hizi hayo hayapo, fedha imekuwa ni njia ya
mkato katika kupata kila kitu. Kwa mwanamke fedha ni mtego umnasao kama
panya na kipande cha nguru mtegoni. Siku hizi ukiwa na fedha una uwezo
wa kumpata mwanamke umtakaye, fedha imekuwa kama tufani, inabeba waliomo
na wasiokuwemo, hata wale watakaotokwa na povu kupinga hoja hii,
nadhani hawajapata bahati ya kukutana na wanaume wenye fedha, laiti
wangepata wasingeweza kusimama hapa na kupinga hoja hii. Kwa ushauri tu,
si vibaya kuangalia mwanaume mwenye muelekeo wa kutafuta lakini hicho
kisiwe ni kigezo namba moja, kwani kama akikuonyesha sifa hizo kabla ya
kuingia kwenye uhusiano kisha ukaingia na baadaye ukagundua mwanaume
huyo si mali kitu wenyewe mnaita mwanaume suruale, utaumia sana.
7. Uzuri wa kitandani
Ninaposema uzuri wa kitandani namaanisha kuridhishana katika tendo la
kujamiiana, kwa kawaida wanawake ndiyo wahanga wakubwa linapokuja swala
la njaa chumbani, wao ndiyo kwa asilimia kubwa hawaridhishwi na wenzi
wao katika tendo. Siyo kwamba waume zao wana udhaifu, la hasha,
inawezekana wanazo nguvu kama za simba, lakini kwa kawaida tendo la
kujamiiana haliwi zuri eti kwa sababu tu mwanaume anazo nguvu kama za
simba, bali inahitaji usanii na utundu ukiwemo werevu wa kihisia kuweza
kumfikisha mwanamke kileleni. Wanaume wengi kwa sababu ya mazoea
wanadhani swala la kumfikisha mwanamke kileleni ni kutwanga kwa kutumia
msuli. Si kweli hata kidogo, ni kumuandaa mwanamke kwa maneno matamu
kabla hata ya kuelekea kitandani. Kwa hiyo wapo wanaume wenye ufundi huo
linapokuja swala la kujamiiana, nia mafundi hodari wenye uwezo wa
kuwafikisha wenzi wao peponi, lakini inawezekana katika maeneo mengine
ya kimaisha wakawa watupu kabisa. Siyo wawajibikaji, wanyanyasaji
wakubwa, hawana staha, hawawaheshimu wenzi wao na ni wenye vurugu
kichwani. Wakati mwingine mwanamke anaweza kunasa kwa sababu hiyo tu, ya
ufundi wa kitandani, lakini akajikuta anaishi katika machungu kutokana
na kutothaminiwa na kunyanyaswa kupita kiasi. Kinachomuweka si kingine
ni ile starehe ya muda mfupi wawapo kitandani tu basi. Kuna haja ya
kujiuliza, Je ni kitu gani hasa kinachokufanya umpende mwenzi wako? Kama
utamkubali na udhaifu wake na una uwezo wa kuhimili hizo tabia
zisizofaa kwa maana kwamba hazikuumizi kihisia (kitu ambacho si rahisi
sana kwa wanawake) ni sawa, lakini kama huwezi, sikushauri kuingia
katika uhusiano wa aina hiyo, kwani ni kujitafutia kaburi la mapema.
0 comments:
Post a Comment