Mwanamuziki Hafsa
Kazinja anayetamba na Wimbo wa Mlala Nje huku video yake ikiwa tayari,
ameamua kuikacha dini yake ya Kiislam na kuhamia kwenye Ukristo. Hafsa
alisema alifikia uamuzi huo baada ya kusumbuliwa na maruhani ambayo
yalimfanya arukwe na akili.
Mwanamuziki Hafsa Kazinja.
“Niliumwa sana hadi ikaonekana nimerukwa
na akili, maruhani ndiyo yaliyokuwa yananisumbua. Kuna kipindi yalikuwa
yakiniambia nisile samaki wala dagaa, mara yakaniambia natakiwa kuwa
mganga.
“Njia zote ziligonga mwamba, nikaambiwa
nisali na nimuachie Mungu, nikawa nikisali sauti zinanijia nimtukane
Mungu tena matusi makubwa, nimeenda hadi kwa waganga, mashehe na
walokole wakaniombea na nikapoteza pesa nyingi hadi nikauza nyumba yangu
na magari lakini wapi. Nimekwenda Kanisa la Zoe ndiyo nimepona,
namshukuru Mungu.
0 comments:
Post a Comment