Aliyekuwa
kocha mkuu wa Yanga, Mholanzi Van der Pluijm (wa kwanza kulia)
anatarajia kuungana na Mkwasa (wa pili kulia) nchini Saudi Arabia
anatarajia kuungana na Mkwasa (wa pili kulia) nchini Saudi Arabia
KOCHA
msaidizi wa klabu ya Yanga, Mtanzania Charles Boniface Mkwasa ametimkia
Uarabuni kuungana na aliyekuwa bosi wake msimu uliopita Mholanzi, Hans
Van Der Pluijm.
Pluijm
baada ya kumaliza mkataba wake wa miezi sita Yanga, aliamua kuondoka
kwenda Saudi Arabia kuifundisha klabu ya ligi kuu ya Saudi Arabia
iitwayo Al Shoalah FC .
Kocha
huyo Mholanzi aliondoka kwa makubaliano maalum na Yanga, huku akieleza
kuwa wakati anajiunga na Yanga aliwaambia kuna dili anasubiria na kama
litakwenda sawa ataondoka.
Baada ya mambo kwenda sawa, aliondoka Yanga na kuagana kwa amani na uongozi wa Yanga pamoja na wanachama.
Pluijm
alionekana kumkubali Mkwasa na sasa ameamua kumtafutia kazi nchini
Saudi Arabia na kocha huyo Mtanzania anakwea pipa usiku huu.
Kabla ya kukwea pipa, Mkwasa amesema tayari ameshawajulisha viongozi wa Yanga na umetoa Baraka zote na kumpa ushirikiano mzuri.
“Viongozi
wamenipa ushirikiano mzuri kwasababu nao wangependa nipate uzoefu
hususani kwa klabu za nje. Labda nitakaporudi nitaweza kuisaidia klabu”.
Alisema Mkwasa.
Hata
hivyo, Mkwasa amegoma kutaja timu anayoenda kufanya kazi kwasababu
mambo hayajakamilika, lakini mambo yakienda sawa ataanika kila kitu kwa
wananchi.
Mkwasa
aliongeza kuwa yeye amepata mwaliko baada ya kutuma wasifu wake (CV),
ingawa amekiri kuwa hayo yamejiri kutokana na jitihada za aliyekuwa
kocha wa Yanga, Hans Der Pluijm.
Kocha
huyo aliyekuwa na Ruvu Shooting mwanzoni mwa msimu uliopita aliongeza
kuwa Saudia Arabia ipo juu kisoka ukilinganisha na Tanzania na kizuri
zaidi wachezaji wengi wa ulaya wanapochoka huwa wanatafuta nafasi ya
kucheza huko, hivyo itampa changamoto mpya.
Mkwasa
alifafanua kuwa mashabiki wa Yanga wasiwe na wasiwasi kwasababu anaenda
kujifunza huko na kuna uwezekano akapangiwa majukumu tofauti na
aliyokuwa nayo sasa hivi.
“Naenda kupata uzoefu ambao naamini nitakapoupata, naamini utaisaida Yanga na taifa kwa ujumla”. Alihitimisha Mkwasa.
Kila la heri Charles Boniface Mkwasa `Master` katika maisha mapya ya kazi yako huko Uarabuni.
0 comments:
Post a Comment