Waziri
Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema vijana 10,500 waliojitokeza hivi
karibuni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kufanya usaili wa nafasi
70 za kazi katika Idara ya Uhamiaji, ni ishara kuwa bomu la ajira
litalipuka muda wowote.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana nje ya Viwanja vya Bunge, Lowassa alisema
Serikali ni lazima ihakikishe inatengeneza ajira kwa kuwa kila mwaka
zaidi ya vijana 30,000 wanahitimu katika vyuo mbalimbali nchini.
Wasomi
hao wa fani mbalimbali walijitokeza katika uwanja huo Ijumaa iliyopita,
kuanzia saa 12 asubuhi wakisubiri kufanyiwa usaili huo.
Lowassa
ambaye alijiuzulu wadhifa wa Waziri Mkuu mwaka 2008, amenukuliwa mara
nyingi akiitaka Serikali kuchukua hatua kukabiliana na tatizo la ajira
na akisema ni bomu linalosubiri kulipuka.
Mbunge
huyo wa Monduli kupitia CCM, aliwahi kuingia kwenye malumbano makali na
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka kuhusiana na suala la ajira
kwa vijana.
Kabaka
akiwa bungeni, Machi 21, 2012 alitoa takwimu za namna Serikali
ilivyokuwa inatengeneza ajira kwa nia ya kumjibu Lowassa, ambaye alikuwa
ameeleza tatizo la ajira linavyowaathiri vijana.
Jana, Lowassa kuongezeka kwa makundi ya vijana wanaopora watu katika maeneo mbalimbali nchini ni ishara ya ukosefu wa ajira. “Watanzania
sasa tupo milioni 48 na kila mwaka vijana zaidi ya 30,000 wanahitimu
vyuo vikuu na kazi hakuna, pamoja na hilo hatuambiwi ni vijana wangapi
ambao hawana kazi,” alisema Lowassa.
Alisema
lazima Serikali itengeneze ajira kwa wananchi wake, huku akimtolea
mfano Rais wa Marekani, Barack Obama kwamba alishinda awamu ya pili kwa
sababu ya kutengeneza ajira.
“Mfano
mzuri ni katika uanzishwaji wa viwanda. Tunapofikiria kuanzisha kiwanda
cha pamba kwanza lazima tuangalie tutatengeneza ajira ngapi,” alisema.
Katika
kuonyesha kuwa ajira sasa ni tatizo nchini, juzi jioni wakati wa
mjadala wa Bajeti Kuu, Naibu Spika Job Ndugai alisema Mtanzania mwenye
nia ya kugombea urais mwaka 2015 ili aweze kuelekewa kwa wananchi ni
lazima aeleze mikakati ya kuwasaidia vijana kupata ajira.
“Ajira
ni tatizo kubwa na lazima lishughulikiwe. Kuna vijana hawaendi shule
lazima watazamwe. Kuna wanaomaliza darasa la saba, kidato cha nne, cha
sita na vyuo vikuu.
Nazungumza kutoka moyoni kabisa. Hizi ni dakika za mwisho za Serikali ya awamu ya nne, wale wanaojipanga kwa awamu ya tano kama hawataongelea ajira basi waandike wameumia.”
Nazungumza kutoka moyoni kabisa. Hizi ni dakika za mwisho za Serikali ya awamu ya nne, wale wanaojipanga kwa awamu ya tano kama hawataongelea ajira basi waandike wameumia.”
Ndugai alisema vijana wasio na kazi ndiyo wapigakura wakubwa na kusisitiza kuwa mgombea yeyote makini ni lazima afikirie suala la ajira kwa vijana.
Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe alisema: “Vijana 10,500 kufanya usaili wa nafasi 70 ni janga la taifa. Yupo kiongozi mmoja mwandamizi wa CCM aliwahi kulizungumza hili lakini akapondwa kwamba anazungumza mambo kwa kuzua. Sasa huu ndiyo ukweli wenyewe.”
0 comments:
Post a Comment