Polisi wamefanikiwa kumnasa mwanamke anayedaiwa kumtesa kwa kipigo na
kumng’ata mtoto Merina Mathayo (15), kumsababishia majeraha makubwa kichwani.
Kamanda
wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Camillius Wambura akizungumza na
Mwananchi jana alisema walifanikiwa kumnasa juzi, mwanamke huyo akiwa
mafichoni Mbagala wilayani Temeke.
“Tumefanikiwa kumnasa juzi usiku akiwa mafichoni kwa jamaa zake,
ni mwanasheria wa kujitegemea ana umri wa miaka 44, lakini inashangaza kwa hayo aliyoyatenda, anaendelea kuhojiwa wiki ijayo tunatarajia kumpandisha kizimbani,” alisema Wambura.
Mtuhumiwa
huyo ambaye ni mkazi wa Boko, anadaiwa kumtesa mtoto huyo ambaye ni
mtumishi wake wa kazi za nyumbani, ambaye sasa amelazwa katika wodi ya
dharura ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa(MOI) Muhimbili Dar es Salaam.
Wakati
huo huo, Uongozi wa MOI umejizatiti kulinda usalama wa mtoto huyo, kwa
kuzuia vyakula kutoka nje ya taasisi hiyo, ikiwa ni pamoja na kudhibiti
watu kumtembelea na kuzungumza naye.
Mmoja wa wauguzi katika wodi aliyolazwa alieleza mtoto huyo kwa sasa anahudumiwa kila kitu na taasisi hiyo.
Ofisa
Uhusiano wa MOI, Patric Mvungi , alieleza kwamba majibu ya kipimo
kikubwa cha CT Scan alichofanyiwa yametoka, ambapo yameonyesha hakuna
mfupa uliovunjika kichwani.
Mtoto
Merina amelazwa Moi baada ya kupewa rufaa na Hospitali ya Mwananyamala
alipokuwa amelazwa awali, kutokana na majeraha hayo ya kung’atwa meno na
kupigwa na vitu mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment