Mfanyakazi wa ndani, miaka 14 mkazi wa
kijiji cha Mdenge, Kata ya Likombe katika Wilaya ya Mtwara, amebakwa na
mwajiri wake usiku wa kuamkia jana na kumsababishia maumivu makali na
kisha kutokomea kusikojulikana.
Akiongea jana Jumatatu Juni 16, 2014,
Mama mzazi wa mtoto huyo, mwenye umri wa
miaka 36, amesema mtoto wake amekumbana na masahibu hayo siku nne tangu aanze kufanya kazi kwa mwajiri wake aliyemtaja kwa jina moja la, Sharifu (42), mfanyakazi katika kiwanda cha kuzalisha saruji cha Alosko mkoani humo.

Amebainisha kuwa, mtoto wake alipata
kazi ya kufanya kazi za ndani kwa mwajiri huyo Juni 12, 2014 ambapo
ilipofikia usiku wa kuamkia leo mtoto huyo aliamua kutoroka nyumbani kwa
mwajiri wake anayeishi na mke wake bila kuaga kutokana na hofu ya
kuzuiwa kwenda kwao au kufanyiwa unyama zaidi na kukimbilia nyumbani
kwao.
“Alivyopata kazi anasema hii sio mara
ya kwanza kufanyiwa hivyo hii ni mara ya pili, usiku wa kuamkia
Jumamosi ya Juni 14, 2014 alimuingilia mtoto wangu na alipomwambia
atatoa taarifa akamwambia asiseme kwa mtu yeyote kwani atamfanya kama
mtoto wake, sasa leo tena amemuingilia.
“Nimemkuta yule mama aliyekuwa
anafanya kazi kwake amesema alihisi kuwa kuna huo mchezo lakini aliogopa
kuniambia tangu Jumamosi” alisema mama wa mtoto.
Kwa upande wa mtoto huyo, amesema ,“Nilikuwa
nimelala usiku wa manane ndipo niliposhtuka, nilipotaka kupiga kelele
alinikataza kuwa nisiseme kwa mtu kwani atanifanya kama mtoto wake, na
usiku wa kuamkia leo alikuwa ameenda kuangalia mpira nilivyoshtuka
alikuwa ameniingilia kimwili ndio nikaondoka asubuhi kwenda kwetu kwa
maana alisema nisipige kelele”
Taarifa yatolewa Polisi
Mama mzazi wa mtoto huyo amesema wameripoti tukio hilo katika Kituo cha Polisi Mtwara, kwa tuhuma hizo na amefunguliwa jalada namba Mt/RB/2198/2014 ambapo mtoto huyo amefanyiwa vipimo katika kituo cha Polisi kilichopo wilayani humo na kugundulika kuwa alibakwa na kupata majeraha makubwa.

Mtandao ulimtafuta Kamanda wa Polisi wa
mkoani humo, Zelothe Stephen, ambaye hakupatikana kupitia simu yake ya
mkoni baada ya kuita bila kupokelewa, huku upande wa ndugu wa mtuhumiwa
wakigoma kuongelea suala hilo wakidai hawajui alipo ndugu yao licha ya
kushangazwa na tukio hilo.
0 comments:
Post a Comment