MKAZI wa Yombo Kilakala jijini Dar es Salaam, Charles Swai (48), amekutwa chumban
i kwake akiwa amefariki dunia.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP), Englibert Kiondo, alisema tukio hilo lilitokea majira ya saa 8:00 mchana, ambapo mwili wa marehemu ulikutwa kitandani na haukuwa na jeraha lolote.
Kiondo alisema kifo hicho kiligundulika baada ya Swai kutofungua mlango wa chumba chake tangu alipofunga Julai 23 saa 2 usiku, ndipo majirani walipochungulia dirishani na kumuona akiwa amelala na kutoa taarifa Kituo cha Polisi Chang’ombe.Alisema askari walifika eneo hilo na kuvunja mlango na kumkuta akiwa amefariki dunia. Chanzo cha kifo hakijafahamika na mwili umehifadhiwa hospitali ya Temeke. Upelelezi unaendelea.

Katika tukio jingine, dereva aliyefahamika kwa jina la Felix Mgoba (25) mkazi wa Wazo, amefariki dunia baada ya gari alilokuwa akiendesha kugongana na Fuso. Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Kamishna Msaidizi (ACP), Camillius Wambura, alisema lilitokea juzi saa 5:20 asubuhi huko barabara ya Bagamoyo eneo la Boko Msikitini.
0 comments:
Post a Comment