SAKATA la
mtoto Devota Malole mwenye umri wa miaka mitano, ambaye ni mlemavu
aliyeibuliwa baada ya kufichwa chini ya uvungu wa kitanda kwa muda wa
miezi mitatu huko Matongolo, Dumila,Tarafa ya Magole wilayani Kilosa
limeibua mambo mapya, baada ya kubaini kuwa aliyesababisha kuokolewa ni
mume wa mama wa binti huyo.
Mashuhuda waliokuwepo wakati wa
kufichuliwa kwa mtoto huyo, wakiwemo majirani na wapangaji wa nyumba
aliyokuwa akiishi, walisema mpangaji wa chumba hicho, Masumbuko Mkwama
(25), aliishi peke yake kwa muda mrefu kabla ya miezi mitatu iliyopita,
kuja na mwanamke aliyemzidi umri, Salah Mazengo (36) aliyemtambulisha
kama mke wake akiwa na watoto watatu.
Msimamizi wa nyumba hiyo, Donata Sisie
ambaye alidai mwenye nyumba anaishi Morogoro mjini, alisema baada ya
kumuhoji mwanamke huyo, alisema alikuwa na watoto watano na kila mmoja
alikuwa na baba yake na kwamba watatu kati yao, walichukuliwa na wazazi
wao na hivyo kubaki na wawili, Elias mwenye umri wa miaka nane na mdogo
wa mgongoni.
“Juzi Julai 8, Masumbuko aliwafuata
wapangaji wenzake watatu na kuwaeleza kwamba mkewe ana mtoto mlemavu
ambaye ni mgonjwa, lakini mwanamke huyo hataki mwanaye atibiwe, jambo
ambalo linamshangaza. Kwa pamoja, watu hao walikwenda kutoa taarifa kwa
Mwenyekiti wa Kitongoji, ambaye baada ya kuelezwa juu ya mtoto huyo,
aliamua kwenda polisi.
“Julai 10, mwaka huu, askari polisi
pamoja na mwenyekiti huyo walikuja hapa nyumbani na kumfichua mtoto huyo
chini ya uvungu. Tokea siku ya tukio, Masumbuko hajulikani alipo.
“Juzi ulitokea mvutano mkali hapa kwani mama mzazi wa Sala alifika akitaka kuchukuwa vyombo vilivyomo ndani ya chumba cha Masumbuko, mimi nilimzuia kwa hoja kwamba ninachojua chumba ni cha mvulana hivyo nimevichukua vitu vyake na kuvihifadhi kwangu hadi atakapofika.”
“Juzi ulitokea mvutano mkali hapa kwani mama mzazi wa Sala alifika akitaka kuchukuwa vyombo vilivyomo ndani ya chumba cha Masumbuko, mimi nilimzuia kwa hoja kwamba ninachojua chumba ni cha mvulana hivyo nimevichukua vitu vyake na kuvihifadhi kwangu hadi atakapofika.”
Mmoja wa wapangaji wenzake na Masumbuko,
Asha Mohamed alisema alipohamia yeye na mumewe, walimkuta Masumbuko
akiishi peke yake hadi miezi mitatu iliyopita walipomuona akimleta
mwanamke mtu mzima aliyekuwa na watoto watatu, mmoja akiwa na ulemavu wa
miguu.
Alisema alimuona mtoto mlemavu akiwa salama kwa siku moja tu, ile aliyofika na tangu hapo hakumuona tena.
Alisema alimuona mtoto mlemavu akiwa salama kwa siku moja tu, ile aliyofika na tangu hapo hakumuona tena.
“Alipokuja alikaa naye hapa kwenye
korido, sijamuona tena hadi juzi alipofichuliwa akiwa tofauti na
nilivyomuona mwanzo, kiukweli huyo mtoto alizaliwa akiwa mlemavu na kwa
mujibu wa maelezo ya mama yake, baba yake alimkana baada ya kumuona na
ulemavu.
“Niwe mkweli kwenye hili, mtoto huyu
alifichwa uvunguni tangu ahamie hapa, hii inatokana pengine na ugumu wa
maisha kwani kwenye chumba chao wana kitanda futi nne na wanalala wanne
baba, mama mtoto wao mkubwa Elias na huyo mtoto wa mgongoni, kuna
kipindi nilimuuliza Devota alikuwa wapi aliniambia kuwa alimpeleka kwa
bibi yake yaani mama yake anayeishi kitongoji kinachofuata,” alisema
Asha.
Juu ya kazi za wazazi hao wawili,
Hambosi alisema mwanaume anauza mishikaki na mwanamke pombe za kienyeji
katika kilabu cha pombe za kienyeji.
0 comments:
Post a Comment