Thursday, 31 July 2014

PICHA ZA FUMANIZI:MKE WA MTU AFUMWA LIVU NA MWANAMME MWINGINE CHUMBANI KWA MUMEWE MCHANA KWEUPE


Mwanamke aliyetambulika kwa jina moja la Mwanahamisi au mama Daudi, mkazi wa Pugu-Kajiungeni, Dar, amejikuta akipata aibu ya karne baada ya kudaiwa kuingiza mwanaume mwingine chumbani kisha kufumaniwa na mumewe.

MSAMAHA: Mwanahamisi ambaye ni mke wa mtu akiomba samahani baada ya kunaswa.

Tukio hilo la kufedhehesha lilijiri hivi karibuni, mchana kweupe nyumbani kwa wanandoa hao maeneo hayo.

ILIKUWAJE?
Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa wanandoa hao, mume wa Mwanahamisi aitwaye Mashaka au baba Daudi ana rafiki yake aliyetajwa kwa jina moja la Paulo ambaye alidai kusumbuliwa na shemeji yake (mama Daudi) kwa muda mrefu.
Ilidaiwa kuwa mama Daudi alikuwa akimtumia Paulo ujumbe wa mapenzi kupitia simu hadi wakati mwingine kufikia hatua ya kumbana na kumkumbatia pale anapokutana naye njiani.
Ikaelezwa kwamba Paulo alimwambia baba Daudi kuwa alikuwa ameshamtumia zaidi ya SMS 240 za kimapenzi.
Baada ya kuona kero zimezidi huku rafiki yake akimlalamikia kutomuelewa mke wake aliyezaa naye mtoto mmoja ambaye bado hata hajaacha kunyonya, Paulo aliamua kuvunja ukimya na kumuonesha ujumbe anaotumiwa na shemeji yake huyo ili wamkomeshe.


AIBU YA USALITI: Mke wa mtu pamoja na njemba aliyokuwa nayo wakiwa na aibu baada ya kunaswa live chumbani.
Ilisemekana kwamba baada ya kufanya tathmini ya SMS hizo, baba Daudi na Paulo waliweka mtego huku wakimshirikisha mke wa Paulo ambaye aliwahi kugombana na mama Daudi kwa kitendo cha kumtambia ovyo.
Ilielezwa kuwa baada ya mpango kukamilika huku Paulo akimwambia shemeji yake kuwa amemkubalia, mama Daudi alimuaga mumewe kuwa baba yake ni mgonjwa huko Yombo-Buza, Dar hivyo anakwenda kumuona na siku hiyo atarudi saa 12:00 jioni akijua kuwa kwa mwanya huo ataweza kwenda gesti maeneo ya Ukonga-Mombasa, Dar na Paulo kama walivyokubaliana.
Ilisemekana kuwa baada ya Paulo kuona gesti patakuwa na shida ya kumshikisha adabu mama Daudi, alimshawishi wakutane chumbani kwa mumewe (baba Daudi) ili iwe rahisi kumfumania.
Ilifahamika kwamba ili kusaliti chumbani kwa mumewe, alimpigia simu baba Daudi kujua alipokwenda.
Kwa kuwa baba Daudi alijua mchezo, alimwambia mkewe kuwa amekwenda kufuatilia kitambulisho cha kazi kisha atakwenda Kigogo, Dar kwenye mishemishe nyingine.
Ilidaiwa kuwa majibu hayo yalimfurahisha mama Daudi ambaye alimwalika Paulo chumbani kwa mumewe bila kujua aliwekewa mtego.

KIPONDO: Mke wa mtu akipokea kichapo baada ya kubambwa.

SAA 7:OO MCHANA KWEUPE
Mishale ya saa 7:00 mchana, Paulo aliondoka nyumbani kwake na kuwaacha wafumaniaji wakiwa tayari, alipofika kwa mama Daudi naye akainua simu kumpigia baba Daudi kumhakikishia Mwanahamisi kuwa mume wake harudi muda huo, akamwambia kuwa amekwenda mbali wataonana saa 12:00 jioni.
Ilidaiwa kuwa ili wafaidi mambo vizuri, mama Daudi alimuondoa mtoto wake na mdogo wake kwa kuwapa fedha ya kwenda kulipia kuangalia ‘tiivii’ kibandani ili abanjuke na Paulo kwa raha zake.
Nusu saa kabla ya tendo, Mwanahamisi alikuwa ameshasaula nguo zote mwilini ndipo Paulo alipomtaarifu baba Daudi kuwa mchezo tayari anaweza kufumania.

OFM, BABA DAUDI
Baba Daudi, huku akiambatana na makamanda wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers alitimba chumbani kwake na kumbamba mkewe ‘live’ kitandani kwake, tayari kusaliti ndoa.
Huku OFM ikishuhudia, mama Daudi alishtuka na kukimbilia khanga kisha akaanza kutoa lawama kwa Paulo kwa kumtia mtegoni.
Katika utetezi wake, mama Daudi alilia kwa uchungu na kusema kuwa ni shetani na tamaa ya fedha ndiyo iliyomponza kwani alijua angelamba mshiko kutoka kwa Paulo.
“Yaani naumia sana kwa mume wangu kunifumania tena na rafiki yake, naomba msamaha, ni shetani tu alinipitia,” alisema mama Daudi huku akimpigia magoti baba Daudi.
Pamoja na utetezi wake, mama Daudi alikula kichapo cha nguvu kutoka kwa mke wa Paulo ambaye aliunganishwa kwenye mtego.
Baada ya mtiti wa nguvu, mama wa Mwanahamisi aliitwa ambapo alipofika na kujionea aibu ya mwanaye, presha ilimpanda, akashindwa kuongea. Hata hivyo, fumanizi hilo liliisha baada ya mmoja wa majirani kusuluhisha ugomvi huku akiwaongoza ibada ya toba kisha akawaomba wasameheane.
Mwanahamisi akamuangukia mumewe na kumuomba msamaha, maisha yakaendelea

You might also like:

0 comments:

Post a Comment