MTU
MMOJA ASIYEFAHAMIKA JINA, JINSI YA KIUME, MWENYE UMRI
KATI YA MIAKA 26 – 30 AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.320 AQV AINA YA TOYOTA COASTER LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE OMARY KASYUPA (46) MKAZI WA KIWILA – TUKUYU.
KATI YA MIAKA 26 – 30 AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.320 AQV AINA YA TOYOTA COASTER LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE OMARY KASYUPA (46) MKAZI WA KIWILA – TUKUYU.
TUKIO
HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 18.07.2014 MAJIRA YA SAA 07:30 ASUBUHI
KATIKA ENEO LA MWISHO WA MJI, KATA YA BAGAMOYO, TARAFA YA TUKUYU MJINI,
WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA CHANZO CHA AJALI HIYO NI
MWENDO KASI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA MAKANDANA –
TUKUYU. DEREVA AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUONI.
KAIMU
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL N.
MASAKI ANATOA WITO KWA MADEREVA NA WATUMIAJI WENGINE WA VYOMBO VYA MOTO
KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO HIVYO HASA KWA KUZINGATIA SHERIA NA
ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
AIDHA ANATOA WITO KWA WATUMIAJI WENGINE WA BARABARANI HASA WATEMBEA KWA
MIGUU KUVUKA KATIKA MAENEO YENYE VIVUKO NA KUTEMBEA PEMBEZONI MWA
BARABARA.
TAARIFA ZA MISAKO:
MSAKO WA KWANZA:
WATU
WAWILI WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA UPENDO WILAYA YA CHUNYA WALIOFAHAMIKA
KWA MAJINA YA 1. KURUSUMU KALUKALA (36) NA 2. MATILDA TUSKER (24)
WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA BAADA YA KUKAMATWA WAKIWA
NA POMBE HARAMU YA MOSHI UJAZO WA LITA 90.
WATUHUMIWA
WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 18.07.2014 MAJIRA YA SAA 07:10 ASUBUHI HUKO
KATIKA KITONGOJI CHA MALANGALI, KIJIJI CHA UPENDO, KATA YA MAMBA, TARAFA
YA KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. WATUHUMIWA NI
WAPIKAJI/WATENGENEZAJI NA WAUZAJI WA POMBE HIYO.
KATIKA MSAKO WA PILI:
MTU
MMOJA MKAZI WA KITONGOJI CHA MACHINJIONI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA
MELLAMA RICHARD (52) ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA BAADA
YA KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA SABA (07).
MTUHUMIWA
ALIKAMATWAMNAMO TAREHE 18.07.2014 MAJIRA YA SAA 11:48 ASUBUHI HUKO
KATIKA KITONGOJI CHA MACHINJIONI, KIJIJI NA KATA YA MKWAJUNI, TARAFA YA
KWIMBA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA BAADA YA KUFANYIKA MSAKO KATIKA
MAENEO HAYO. MTUHUMIWA NI MTENGENEZAJI NA MUUZAJI WA POMBE HIYO.
TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAIMU
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL N.
MASAKI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI
[GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
AIDHA ANATOA WITO KWA WANANCHI KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ZA
MTU/WATU AU KIKUNDI CHA WATU WANAOJIHUSISHA NA UTENGENEZAJI NA UUZAJI WA
POMBE HIYO ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
Imetolewa na:
[BARAKAEL N. MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Imetolewa na:
[BARAKAEL N. MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment