Monday, 11 August 2014

JACK PATRICK AYEYUKA GEREZANI, TIRIRIKA NA STORI NZIMA HAPA


Nini kinaendelea? Video Queen wa Bongo anayeshikiliwa na jeshi la polisi nchini China kwa msala wa madai ya kukamatwa na madawa ya kulevya ‘unga’, Jacqueline Fitizpatrick Cliff ‘Jack Patrick’ anadaiwa kuyeyuka gerezani.
Video Queen wa Bongo, Jacqueline Fitizpatrick Cliff ‘Jack Patrick’.

Kwa mujibu wa ‘mtu wetu’ aliyeambatana na rafiki zake Jack kwenda kumuona gerezani, Macau, Hong Kong nchini humo, walijikuta wakipigwa na butwaa kuambiwa hakuna mtu kama huyo gerezani hapo hivyo kuibua hofu kuwa huenda amenyongwa.
Uchunguzi wetu gerezani hapo ulibaini kwamba tofauti na hofu ya rafiki zake, kuna uwezekano Jack amehamishiwa gereza lingine lililopo nje kidogo ya Mji wa Macau.Chanzo chetu hicho kilidai kwamba habari za ndani zilieleza kwamba Jack amehamishwa gereza hivyo kwa maelezo zaidi watu wanaokwenda kumtembelea waende kwenye ofisi za gereza hilo alilokuwa awali watapewa maelekezo wapi alipo mtu wao.
Jacqueline Fitizpatrick Cliff ‘Jack Patrick’ akiwa Chini ya ulinzi mkali China.
“Unajua watu wanaokwenda kumtembelea Jack gerezani ni Watanzania walioko huku China kwa shughuli maalum hasa za sanaa, kama vile sarakasi au maigizo, wengine wote wanaogopa, wanajua wanaweza kukamatwa.
“Tulipokwenda na mazagazaga yetu tuliambiwa Jack amehamishwa gereza na inaonekana aliomba mwenyewe ila hatujui ni kwa nini alifanya hivyo,” kilisema chanzo hicho.Hivi karibuni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, John Haule alitoa taarifa na kutaja jumla ya watuhumiwa waliokamatwa kwa kesi za madawa ya kulevya ambapo alisema kuwa kuna Watanzania wengi wapo kwenye magereza mbalimbali China.


“Katika magereza ya China hadi Februari (mwaka huu) tulipewa taarifa kwamba wapo Watanzania 177 magerezani na kati ya hao 15 wamehukumiwa kunyongwa kutokana na baishara hiyo ya madawa ya kulevya,” ilisema taarifa hiyo ya katibu mkuu.
Jack alikamatwa Macau, Hong Kong, mwaka jana hivyo kesi yake inaendelea kuunguruma. Tofauti na Beijing ambao huwa wananyonga watu wanaojishughulisha na unga, Hong Kong ni kifungo cha miaka kadhaa tu.

0 comments:

Post a Comment