Tuesday, 19 August 2014

JINSI YA KUZUIA MAUMIVU WAKATI NA BAADA YA TENDO.



Maumivu haya wakati na baada ya tendo hutokea wakati wa tendo au
baada ya tendo la ndoa na husababishwa na matatizo mengi katika njia ya uzazi. Kama maumivu yanatoka ndani kabisa ya nyonga huweza kusababishwa na maambukizi katika via vya uzazi(PID) na uvimbe.
Kuvimba au maambukizi ya njia ya mkojo(UTI) na Zinaa kama Chlamydia usababisha maumivu ndani ya uke na kwenye shingo ya kizazi. Majeraha na kuumia kwa sehemu za uke au uume usababisha maumivu  sehemu za nje na ndani ya uke wakati na baada ya tendo.
Maumivu juu na katika ngozi ya sehemu za siri husababishwa na maambukizi ya fangasi au vipele na makovu sehemu za siri.Kukosa maandalizi ya kutosha kabla ya tendo hufanya misuli ya uke kukaza kusababisha maumivu makali wakati na baada ya tendo.


MATIBABU YAKE.
Kama maumivu ni makali sana na ya muda mrefu fika hosipitali ukapime na kutibiwa magonjwa yanayosabisha maumivu haya au unaweza kujaribu kufanya yafuatayo:-
  1. Kuwa na maandalizi ya kutosha kabla ya tendo sambaba na mazoezi yanayosaidia sehemu za siri na nyonga kupumzika na kuwa tayari kwa tendo
  2. Badili mkao unapoisi maumivu asa kwa kukaa juu ya mweza unaweza kupunguza maumivu
  3. Usifanye tendo mpaka pale utakapopata hisia za kutosha
  4. Unaweza kutumia vilainisha vyenye estrojeni kwa ajili ya kulainisha na kuongeza hamu ya tendo

 USIKOSE KUTEMBELEA BLOG HII KILA SIKU KWA MSAADA ZAIDI NA USHAURI.

0 comments:

Post a Comment