Tumekwisha! Taarifa ikufikie kwamba wanaume tata ambao si riziki (mashoga) na wanawake wanaojishughulisha na mapenzi ya jinsi moja (wasagaji) kutoka nchi mbalimbali wamefanya mkutano wao mkubwa wa kimataifa jijini Dar, Ijumaa Wikienda lina mkanda mzima.
Baadhi ya Mashoga wakipata ukodaki.
Bila kujua anazungumza na mwanahabari wetu, mmoja wao alipoulizwa nini kinaendelea hotelini hapo, alisema mkutano huo unawahusu mashoga na wasagaji huku akibainisha kwamba unafanywa kwa siri kubwa.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba.
Baada ya kupata taarifa hizo, kachero wa Ijumaa Wikienda alizama ndani kimafia ambapo alinasa mazungumzo ya kikao hicho, ajenda kubwa ikiwa ni kuishinikiza serikali itambue uwepo wao hapa nchini.Ili kujua kama wizara inajua kinachoendelea, gazeti hili lilimtafuta Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba lakini simu yake iliita bila kupokelewa hivyo jitihada zinaendelea.
0 comments:
Post a Comment