Mhhhh! Baada ya kuwa mpweke kwa muda mrefu, uzalendo ulinishinda nikaamua angalau na mimi nitafute binti wa kuniliwaza. Mchakato huu ulianza kwa binti mmoja ambaye tulikutana kwenye dala dala tukitoka Posta kuelekea Mwenge. Nilivutiwa na mwonekano wa Binti huyu nikaamua niombe namba ya simu.
Mungu si athumani alitoa namba bila hiyana! Kutokana na furaha ya
kupewa namba sikuweza kuongea chochote siku hiyo kama mtu aliyewekewa matambala ya nguo mdomoni hadi muda wa kushuka Mwenge ambapo tuliagana tu na nikamuahidi kumtafuta. Kwa mwonekano, binti huyu ni mwembamba, ana baby face, mweupe wastani pia ni mrefu kidogo. Alikuwa na SmartPhone ya Nokia ambayo gharama yake nakisia sio chini ya Laki Tatu!
Pia alikuwa amejitupia micheni siku hiyo, cjui ya madini gani mshamba mie. Msije Mkaniomba Picha! Sina. Tulianza mawasiliano ya hapa na pale huku nikijaribu kumuonesha kwamba najali. Urafiki wetu ulidumu kwa muda kama wa mwezi mmoja ndipo nilipoamua kumtamkia wazi kwamba ……………….!
Katika urafiki wetu nilipata kujua kwamba binti yule alikuwa anasoma Procurement kwenye chuo Fulani hapa hapa Mjini. Nilizungushwa kukubaliwa ombi langu kwa muda kama wa mwezi mmoja. Sikukata tamaa kwa sababu nawajua watoto wa kike: Kwanza kukubali moja moja ni udhaifu na pia mapozi kwa mtoto wa kike ni ya muhimu kama ilivyo tendo la ndoa kwa walio oana. Baada ya kubembeleza sana ombi langu lilikubaliwa na nikawa rasmi mpenzi wa Fulani.
Kukubaliwa huko kulileta Joto na Raha ndani ya moyo wangu! Kusema kweli nilifurahi wiki ya kwanza huku nikishindwa kujenga taswira kwenye ubongo wangu siku ya kugegedana itakuwaje?????????!!!!. Kitumbua kiliingia mchanga baada ya kuombwa Laki Moja ili aongezee kwenye ada alipe chuo. Nilijiuliza maswali mengi ambayo yalikuwa hayana majibu. - Kwanza kwa nini asimuombe mzazi wake. Mi sio mzazi!!!!! - Miaka yote nani alikuwa anamlipia ada? - Kama mimi nisingekuja kwenye maisha yake, nani angelipa hicho kiasi cha ada! Na mengine mengi. Labda wana MMU mnisaidie kumjibia. Nilitoa laki moja kwa shingo upande. Baada ya hapo nimekuwa mtu wa kupigiwa simu, mara dia sijala, mara dia naumwa naomba hela niende hospitali.
Nimegeuzwa ----- mie kila siku natoa hela tu. Siku alipokuja kunichosha ni pale aliponiambia kwamba SmartPhone yake imetumbukia kwenye maji na imezima kabisa haitaki kuwaka kwa hiyo kwa sasa ameweka kadi ya simu kwenye simu ya mwenzake. Kama umesoma “Critical Thinking and Argumentation” inabidi uwe umeshatambua kwamba nilitakiwa kukununua SmartPhone nyingine labda ya gharama Zaidi kuliko ile aliyokuwa nayo mwanzo.
Nikijiangalia mwenyewe natumia Nokia tena yenye tochi – gharama yake haizidi elfu hamsini. Hata hiyo SmartPhone sijui una-touch vipi kwa sababu nahisi siku nikipewa itanishinda kutumia. Nipo hapa hapa mjini ila mshamba haswa wa mambo hayo! Muda huu nilimwambia kwamba sina hela ya kumnunulia simu hiyo. Ila siku hizi huwa namkuta na Samsung Galaxy S3 Mini. Baada ya kumkatalia kumpa hela ya simu, kwa sasa tunaendelea na mizinga midogo midogo.
Papuchi sijapewa hadi leo. Nikimwita Faragha nijibiwa “Akhu”- msamiati ambao nilikuwa sijawahi kuusikia kabla isipokuwa kwa huyu binti. Penzi letu limekuwa la kukutana pale Mwenge – New Jamarat na kunywa Juisi. Sijawahi hata kugusa kalio mie. Natamani kuachana nae ila roho inaniuma – hela zangu.
Wana MMU naomba mnisaidie kwenye mazingira haya manake naweza nikafa mawazo– angalau nipewe papuchi tu na moyo wangu utapona.
0 comments:
Post a Comment