Wednesday, 20 August 2014

MWANDISHI WA MAREKANI AKATWA KICHWA


Mwandishi wa habari wa Marekani aliyekatwa kichwa, James Wright Foley
(kushoto), akiwa amevishwa kanzu maalum.
Kabla ya kuuawa kwake, Foley, aliwataka marafiki, wanafamilia wake na wapenzi wake wote kupambana na “wauaji wangu wa kweli” ambao ni serikali ya Marekani.
Foley akiwa na muuaji wake ambaye alisema kitendo cha kumwadhibu mwandishi huyo ni kulipiza kisasi mashambulizi ya ndege za Marekani nchini Iraq.

Muuaji wa Foley akijitayarisha kumkata kichwa.
Foley enzi za uhai wake hadi alipopotea Novemba 2012, baada ya kutekwa huko Taftanaz, kaskazini mwa Syria.
Mama yake Foley, Diana, na baba yake John, wakiwa katika mkesha kanisani kuwataka wapiganaji wa ISIS kuwaachia mateka wao.

Kikosi cha Kiislam cha kijeshi chenye msimamo mkali kimeachilia video inayoonyesha mauaji ya mwandishi wa habari mwenye asili ya Marekani, James Foley, aliyepotea tangu alipokamatwa mateka na kushikiliwa nchini Syria miaka miwili iliyopita na sasa ameuawa.

Ikulu ya Marekani imesema inaifanyia uchunguzi wa kina video hiyo na ikithibitika kwamba mwandishi huyo wa habari ni wa taifa hilo, serikali ya Marekani itataka ufafanuzi wa kina ilikuaje na kwa nini James Foley auawe.

0 comments:

Post a Comment