Tuesday, 19 August 2014

NGONO ZEMBE: MSANII WA BONGO FLEVA ANASWA AKINUNUA URODA KWA MACHANGUDOA


WAKATI wasanii wakitakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuenzi maadili mema kwa jamii ya Kitanzania, mambo yamekuwa kinyume, baada ya nyota wa muziki wa kizazi kipya, Ramadhan Shaban 'Wabibi' kukutwa live, akipatana bei na wanawake wanaojiuza katika eneo maarufu kwa machangudoa la Sinza Africasana jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
Nyota wa muziki wa kizazi kipya, Ramadhan Shaban 'Wabibi' akitega
'mingo' kujiopolea machangu maeneo ya Sinza Africasana jijini Dar.

Wabibi anayetamba na kibao chake cha Kitenge kwenye vituo mbalimbali vya redio na runinga nchini, usiku wa saa saba alikuwa akivinjari katika viwanja hivyo, akichagua kama wafanyavyo wateja wa nguo dukani.
Mara baada ya kuonekana kwa msanii huyo katika viwanja hivyo, chanzo chetu ambacho ni kikereketwa cha maadili, kilipiga simu katika ofisi za Oparesheni Fichua Maovu (OFM) kitengo kilicho chini ya Global Publishers saa saba usiku kikiripoti skendo hiyo ya aibu.
Msanii Ramadhan Shaban 'Wabibi' akipatana bei na mmoja wa machangudoa.
Bila kuchelewa paparazi wetu alifika eneo la tukio kwa pikipiki na kumkuta staa huyo akiendelea na chaguachagua yake kwa akinadada waliovalia kihasara ili kuwavutia wanaume wakware.
Mwanga wa kamera zetu hata hivyo haukuonekana kumshtusha sana msanii huyo ambaye alijichekesha na kujifanya kuendelea na shughuli nyingine, kama walivyokuwa wakifanya watu wengine katika eneo hilo linalosifika kwa biashara ya ukahaba jijini Dar.
Ramadhan Shaban 'Wabibi' akiwa na changudoa mwingine.
Baada ya kujipatia picha za kutosha za tukio hilo na kuondoka eneo hilo, makamanda wa OFM hawakwenda kulala, bali waliendelea na uchunguzi wao katika mitaa mbalimbali.Katika hali isiyotarajiwa, saa mbili baadaye, msanii huyo kwa mara nyingine alikutwa na OFM akiwa anaendelea na biashara yake ya sagulasagula ya machangudoa, lakini hivi sasa akiwa amehamishia kambi katika eneo la Sinza ya Mapambano.

Akiwa amevutiwa na mwanadada mmoja na kuanza kufanya naye mapatano ya bei, paparazi wetu alimuwahi kwa kumpiga picha, ambapo safari hii alishtuka zaidi na chapchap, akachukua Bajaj na kutokomea.
'Wabibi' akikurupushwa na kamera zetu za Global katika eneo la tukio.
Wabibi aliwahi kuwa memba wa kundi la muziki la Suba Mkole, akijulikana kama Wambua Classic ambao walitoa albamu iliyotamba kwa jina la Sonde.

0 comments:

Post a Comment