Msanii anayefanya vizuri kunako tasnia ya filamu Bongo, Rayuu Bagenzi ‘Rayuu’ ambaye amewahi kukumbwa na skendo kibao ikiwemo kupiga picha za nusu uchi pamoja na kuonyesha michoro ya tatoo katika sehemu zake nyeti amedai kuwa amelazimika kubadili mwenendo wake hivyo kuomba radhi kwa kuikwaza Familia yake, ndugu, jamaa na marafiki
Rayuu aliamua kuchukua maamuzi hayo baada ya kuona anakoelekea si kwema
hasa katika kujenga msingi wa maisha yake na sanaa kwa ujumla…..Hata hivyo msanii huyo alikana kusambaza picha zake za utupu na kushikilia msimamo kuwa picha hizo zilivujishwa na watu wake waliokuwa na nia ya kumchafua….

“Naiomba radhi familia yangu, ndugu, jamaa na marafiki pamoja na jamii nzima kwa yote niliyofanya.Nimeamua kubadilika na kujitenga na watu wabaya ambao hawanitakii mema. Mimi ni mtu mzima hivyo najua haya ninayoyafanya yatakuja kunigharimu baadae,” alisema Rayuu.
Aliongeza kuwa skendo nyingi chafu zilimdhalilisha na kuleta fedheha katika familia yake na kwamba hahitaji tena kutokea kwa hali hiyo
0 comments:
Post a Comment