Wednesday, 27 August 2014

WAKUBWA TU:JINSI YA KUUFANYA UHUSIANO WAKO UWE WENYE FURAHA SIKU ZOTE...SOMA HAPA



MIGOGORO INATIKISA UHUSIANO, WENGI WANAACHANA, KISA HAPA NI FURAHA! UNAPOKUWA KWENYE UHUSIANO USIO NA FURAHA NI SAWA NA KUJIWEKA NJIAPANDA, INAUMIZA, INATESA SANA.



Nini suluhisho? Jawabu ni kwamba siyo kukimbilia kuachana, inatakiwa uangalie njia nzuri ya kupita ili kumaliza migogoro. Deni kwako ni kubadili hali iliyopo kuwa furaha ya kudumu.


Kuna mambo muhimu ya kujifunza kuhusu furaha yako na amani ya mwenzi wako. Labda kabla sijaenda mbele zaidi, nikufafanulie hili: Sanaa ya busara katika maisha inajumuisha vitu vinne.


Navyo ni NIA na MALENGO. MUNGU ana nafasi yake, hatua chanya na mafanikio endelevu. Ukikaribisha BUSARA kama kanuni yako ya kuishi, maana yake unahitaji amani na furaha. Hilo liweke akilini.

Ukitaka kuishi kwa busara ni lazima uwe na mtazamo wenye furaha. Unapaswa kuiangalia dunia kwa fikra na macho. Furaha; hebu angalia wengine wanavyosononeka kwa kuikosa, kisha jifunze kwa wenye amani.


Mtu sahihi ni yule anayejifunza kupunguza msongo wa mawazo, anayejitahidi kuongeza furaha na kupanua uwezo wake. Kama ndivyo, basi nawe unatakiwa ujiulize: “Utapata vipi furaha ikiwa mwenzio amenuna?”


Akiwa amekasirika utaweza kucheka? Jibu ni kwamba haiwezekani na endapo moyo wako una amani wakati mwenzako amejikunja, ni wazi kwamba penzi lenu ni kama la kwenye sinema. Je, mtaenda hivyo mpaka lini?


Ni vizuri kila mtu ajifunze kupunguza msongo wa mawazo na kuongeza furaha. Ukifanikiwa kuiweka chanya furaha ya mwenzi wako na yako itapatikana. Zingatia msemo kuwa ninyi ni kitu kimoja, wewe ni yeye!


Watu wengi wamekuwa wakishindwa kustawisha uhusiano wao kwa sababu wanashindwa kuishi ndani ya wenzao. Wanatenda mambo ambayo yanawaumiza wenzi wao bila kujiuliza. Hawana malengo chanya.


Mtu mwenye malengo mazuri katika mapenzi ni yule ambaye anajiuliza kabla ya kuzungumza au kutenda. Anatafakari kauli au kitendo na matokeo yake. Pointi kuu ni mapokeo ya mwenzi wake. Ni kosa kufanya tukio lolote au kutoa matamshi yanayoweza kumuudhi mwenzako.


Ni lazima uwe na angalizo kwamba kwako linaweza kuwa dogo lakini kwa mwenzako ni kubwa. Heshimu kosa lolote kwamba linaweza kuhatarisha uhusiano wako, kwahiyo jichunge kila eneo.


Wewe ni mtu tu hapa duniani, inawezekana uzito wako ni mdogo. Ukiwepo na usiwepo taifa halisomi upungufu wowote! Hata hivyo, kupitia mapenzi wewe ni dunia mbele ya mwenzio. Kila kitu hakina thamani kwake bila uwepo wako, kwa hiyo heshimu hisia zake, ingia gharama kumletea furaha.


Mfumo sahihi wa mapenzi ni kuishi ndani ya mwenzako. Kuzijulia hisia zake na kujenga nidhamu ya kuepuka kumpa maumivu yasiyo na sababu. Unaelewa kuwa mwenzako hapendi uchelewe kurudi nyumbani, kwahiyo usifanye makusudi mitaani.


Kuna sababu gani ya kugandana na marafiki mitaani wakati mwenzio amenuna nyumbani? Jiongeze lingine; Mtakapokuwa ‘mnaparurana’ nyumbani hao unaowaendekeza watakuwepo? Si ajabu wakati huo wao wanalala usingizi mzuri, wewe kwako hakulaliki.




Wewe ni mke wa mtu, mambo mengi unachangia naye, ulimwengu ambao unapita naye ni usiku wa giza kwa wengine. Hulioni kama hilo ni maalum? Tambua thamani yake na utekeleze furaha yake.
Kwa kifupi ni kwamba unatakiwa kufanya kila linalowezekana ili mpenzi wako awe na furaha. Wala usiwe mbishi mtoto wa kike; Sifa ya ubabe na kupuuza hisia za mwenzako haiwezi kukusaidia.


Asilimia kubwa ya watu ambao wapo kwenye uhusiano wa kimapenzi, husumbuliwa na tatizo la kutotengeneza penzi. Wakiongozwa na msemo kuwa kila kitu hupangwa na Mungu, nao huacha mapenzi yao yaende kama yalivyo. Hawaamini kuwa barabara ilichongwa, ndiyo magari yakapita.

0 comments:

Post a Comment