Saturday, 20 September 2014

DARASA LA MAPENZI: MWANAMKE UNA UHURU WA KUFUNGUKA KWA MUMEO



Bila shaka ni wazima wa afya na mnaendelea vema na kazi zenu za kulijenga taifa
, kwa wale wagonjwa nawaombea kwa Mwenyezi Mungu inshalla atawaponya na kwa waliokutwa na misiba nawaombea subra ishallah Mungu awapatie moyo wa uvumilivu.

Bila kuwachosha leo nakuja na mada nayingine mpya kwenu mashosti wangu ambao mnajifanya mabubu, hamuwezi kufunguka kwa waume zenu hasa mnapokuwa na haja za kimwili.
 
Shosti kufunguka kwa mumeo kunaleta mapenzi mazito sijui kama mnaelewa kufunguka huko ni  kwa aina gani? Si kwa makosa ee bibie.


Halooo sasa nikueleze tu. Wanawake wameumbwa na haya lakini kwa mumeo hakuna hilo unatakiwa kumwambia mzee nahitaji mambo na ukamuanza mwenyewe usisubiri kuanzwa.


Wewe siku zote kumbuka mume naye anachoka na ataona huna mapenzi naye kwa sababu wahitaji ni wote wawili.

Unataka kuniambia shosti hakuna siku wewe unamhitaji mumeo kwamba ni yeye tu kila siku akuanze?  Sasa wewe bubu nakufundisha kwa njia hii funguka, mueleze mumeo na umuachie mwili atalii kama atakuwa bado hajakukosha mweleze wazi ni wapi akipita anakukosha. Hii inaleta mahaba zaidi, vunja ukimya bibi!


Utakuta mke anaona aibu hata kuchojoa mavazi yake basi mwambie akusaidie kwa sababu nayo ina hamasa yake, mume kuitoa mojamoja mpaka ile ya mwisho muhimu hapo ndipo mahaba yanapoanzia na kuamsha mashamshamu.


Gizani haipendezi, acha mataa yawake kama vile kuna sherehe ili uweze kuiona kila nukta ya mumeo naye aione kila pembe ya mwili wako. Kama hupendi mwanga mkali tumia mwanga hafifu au mishumaa lakini inapendeza zaidi kuujua mwili wa mumeo au mumeo kuujua wako kwa kuuona live si kwa kuhisi gizani. Acheni woga ambao hauna maana mashosti wangu.


Unampapasaje mpenzi/mume/mke kama vile umepoteza kitu kwa sababu ya giza? Huwezi kutambua uzuri aliona mwenza wako kamwe utaishia kumsifia kwa uongo tu.
Sasa basi funguka na uwe huru kwa mwenza wako na uongeze ujuzi muhimu, unaweza kutumia macho, kidevu masikio na pua. Jitume bibi 

0 comments:

Post a Comment