MAHABATi! Beautiful Onyinye wa Bongo, Wema Sepetu ‘Madam’ amedhihirisha kuwa yeye ni mwanamke tayari wa kuwekwa ndani baada ya kusema anajitahidi kila siku katika suala la mapishi ili asimlishe viporo mwandani wake, Nasibu Abdul, ‘Diamond’.
Akipiga domo na paparazi wetu, Wema alisema kama mwanamke anajua thamani ya mwanaume siku zote hata kama ‘baby’ wake atarudi usiku, lazima aingie jikoni kupika na haweki chakula kwenye ‘hot pot’.
“Siku zote si kwamba najisifia ila kwa jikoni ndiyo mwenyewe sasa kwa nini nipike chakula halafu niweke kwenye hot pot? Kwangu siruhusu kabisa itokee,” alisema Wema.
0 comments:
Post a Comment