MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Rashid
Makwiro 'Chid Benz' amekamatwa na madawa ya kulevya aina ya heroine na
bangi akiwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius
Nyerere jijini Dar es Salaam.
Akizungumza Kamanda wa Kuzuia na
Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, SACP, Alfred Nzowa,
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa msanii huyo alikuwa
njiani kuelekea mkoani Mbeya kwa ajili ya shughuli zake za kimuziki.
Kamanda
Nzowa amesema kuwa Chid amekutwa na madawa hayo baada ya upekuzi wa
kawaida uliokuwa ukiendelea uwanjani hapo, ambapo jeshi la polisi
linamshikilia kwa mahojiano na uchunguzi zaidi.
Mara baada ya kupata taarifa hizo,mtandao huu uliwasiliana na Kamanda Nzoa ambaye alifunguka kama ifuatavyo:
Mara baada ya kupata taarifa hizo,mtandao huu uliwasiliana na Kamanda Nzoa ambaye alifunguka kama ifuatavyo:
“Ni kweli tumemkamanda Rashid Makwiro
maarufu kwa jina la Chid Benz akiwa na kete kumi na nne za madawa ya
kulevya aina ya heroine pamoja na misokoto miwili ya bangi.
“Msanii huyo alikuwa njiani kuelekea
mkoani Mbeya kwa ajili ya shughuli zake za kimuziki, na sasa amewekwa
katika sehemu maalum ambayo hatuwezi kusema ni wapi, kwa sababu za
kiusalama, uchunguzi wa tukio unaendelea.”
Taarifa zilizokuwepo awali zilisema kuwa
Chid alikuwa njiani kwenda Mbeya kwa ajili ya kushiriki kwenye shoo ya
Instagram Party ambayo inatarajiwa kufanyika kesho Jumamosi.
Chid ni kiongozi wa kundi la muziki la la Famila lenye makao makuu Ilala jijini Dar es Salaam.
Chid ni kiongozi wa kundi la muziki la la Famila lenye makao makuu Ilala jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment