Je, upo kwenye uhusiano wa kimapenzi, unampenda sana mume, mke, mchumba
au mpenzi uliyenaye lakini wazazi au ndugu zako wanamchukia na kila siku wanampiga vita?
Mada
ya leo ni kwa ajili ya wewe msomaji wangu ambaye upo kwenye mazingira
kama haya ya wazazi au ndugu kumkataa umpendaye kwa sababu ambazo
wanazijua leo. Kwa ambao wamewahi kupitia changamoto hii au bado wapo
ndani yake, watakuwa wanaelewa vizuri ugumu uliopo linapokuja suala kama
hili.
Wazazi
wako wamekuzaa na kukulea tangu ukiwa mdogo mpaka umekuwa mkubwa,
umempata umpendaye lakini wao wanamkataa na kukwambia unatakiwa kuchagua
moja, wao (wazazi) au huyo unayempenda. Utachukua uamuzi gani?
Utamuacha kwa sababu wazazi hawampendi? Utakubali kuwadharau wazazi wako
na kuendelea naye?
Bila
shaka kila mmoja atakuwa na jibu lake tofauti, hata mimi ukiniuliza
nitakuwa na jibu langu lakini tunachokihitaji hapa, ni kujadiliana,
kupanuana mawazo, kupeana uzoefu ili mwisho kila mmoja awe na uwezo wa
kuivuka changamoto hii kwa sababu hata kama bado haijakukuta, huenda ipo
siku na wewe yatakutokea.
MFANO HAI
Hebu soma ushuhuda wa msomaji wangu mmoja ambaye yupo kwenye hali mbaya na anahitaji ushauri:
“Mimi ni mwanaume mwenye umri wa miaka 42, nilioa miaka kumi iliyopita na tumejaliwa kupata watoto wawili. Tatizo linalonisumbua na kuniweka njia panda, mke wangu anawachukia sana wazazi wangu na ndugu wote kutoka upande wangu.“Wazazi wangu wamekuja mjini kwa zaidi ya miezi miwili sasa kwa ajili ya matibabu lakini huwezi kuamini, mke wangu anawachukia kiasi kwamba hata salamu kwake ni mtihani. Anawadharau, wanapishana ndani kama wake wenza, anazungumza maneno machafu dhidi yao ambayo mengine nayasikia, hawapi matunzo mazuri, anawanyanyasa na kibaya anawafundisha mpaka wanangu kuwadharau babu na bibi.

“Hali
hiyo imesababisha wazazi nao waanze kumchukia sana, wananiambia
nimekosea kuchagua mke na wananitolea maneno makali ambayo mengine
hayaandikiki. Nipo njia panda, sijui niamue nini, bado nampenda mke
wangu lakini mambo anayoyafanya yamesababisha mapenzi yangu kwake
yapungue mpaka nafikiria kumpa talaka ili kuwafurahisha wazazi wangu.
Naomba ushauri, nifanyeje?”
Amehitimisha
msomaji wangu huyu, bila shaka umemuelewa. Najua huyu ni mmoja tu
lakini wapo wengi ambao wanatokewa na visa kama hivi. Naomba tujadiliane
pamoja, ungekuwa ni wewe kwenye nafasi ya msomaji huyu, ungefanya nini?
Kama ungepewa kazi ya kumshauri, ungemwambia nini?
TAFUTA CHANZO CHA TATIZO
Hakuna chuki ambayo huwa haina chanzo. Kama mumeo, mkeo anawachukia ndugu zako, jambo la kwanza ambalo unatakiwa kulijua, ni kwamba lazima kuna chanzo kilichosababisha hali hiyo. Na kama yalivyo matatizo mengine yote, huwezi kupata muafaka kama hujakijua chanzo.
Wengi
hushindwa kutumia busara katika kutafuta chanzo. Yawezekana umpendaye
ndiyo chanzo ila kwa sababu ya mapenzi yako kwake, unaukataa ukweli na
kumtetea.
0 comments:
Post a Comment