Watu
sita wakiwamo wahudumu watatu wa afya wa hospitali teule ya Wilaya ya
Sengerema mkoani Mwanza, wamewekwa chini ya uangalizi maalum baada ya kumhudumia mgonjwa aliyefariki akiwa na dalili za ugonjwa wa ebola.Mtu aliyefariki alitajwa kuwa ni Salome Richard (17), anayetoka katika kijiji cha Kahundawilayani Sengerema.Akithibitisha kuwapo kwa hali hiyo Mganga Mfawidhi wa Hospitali Teule ya Wilaya ya Sengerema, Dk. Mary Jose, alisema mgonjwa huyo alifikishwa katika hospitali hiyo na ndugu zake watatu akiwa na homa kali huku akitokwa na damu sehemu mbalimbali za mwili wake.Alisema vipimo vya mgonjwa huyo vimepelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.

“Tulimpokea juzi saa 7 mchana kutoka
katika kijiji cha Kahunda wilayani hapa akiwa na homa kali akitokwa damu
mwilini, lakini kwa tahadhari tulimweka wodi maalum peke yake akipatiwa
matibabu na ilipotimu saa 8 usiku alifariki dunia,” alisema
Alisema kutokana na tahadhari ya ugonjwa
huo, watumishi watatu wa idara ya afya na ndugu watatu wa marehemu
huyo, wamezuiliwa kwa kuwekwa katika uangalizi maalum hadi matokeo ya
vipimo vilivyochukuliwa vitakaporejeshwa toka Muhimbili.
Akizungumzia tukio hilo, muuguzi
Mfawidhi wa hospitali hiyo, Daniel Mihayo, alisema timu maalum ya
watalaam na viongozi wa mkoa walienda hospitalini hapo juzi na kuondoka
na vipimo vya mgonjwa huyo kabla hajafariki dunia kwa kuzingatia
maelekezo ya serikali ya kuchukua tahadhari linapotokea tukio kama hilo.
“Kwa sasa jamii inatakiwa kuepukana na
uzushi uliozagaa kila kona kuhusu mgonjwa huyo kufariki kwa
ebola…tunawamba wasiwe na wasiwasi kwani hatua stahiki zinachukuliwa kwa
wagonjwa wa aina hiyo kama tahadhari,” alisema Mihayo.
Mhudumu aliyempokea mgonjwa huyo katika
hospitali hiyo, Fungameza Majula, alisema ndugu watatu walimpeleka
mgonjwa huyo kwa taksi lakini alipobaini dalili hizo aliujulisha uongozi
wa hospitali na mara moja hatua za tahadhari zilichukuliwa ikiwa ni
pamoja na kuwazuia ndugu kurudi nyumbani.
Hata hivyo, juhudi za kumpata mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Careen Yunusu, kuzungumzia tukio hilo hazikufanikiwa.
Akizungumzia tukio hilo, Mganga mkuu wa
mkoa wa Mwanza, Bw.Valentino Bangi, alisema alipokea taarifa za mgonjwa
huyo kufariki kwa homa inayofanana na ugonjwa wa ebola au maburgh.
Bw.Bangi alisema ofisi yake imetuma timu
ya wataalam wa afya katika Hospitali ya Wilaya Sengerema na kuchukua
sampuli ya vipimo vya mgonjwa na kupeleka Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.
Bw.Bangi alisema ili kukabiliana na
mlipuko wa magonjwa hayo, tayari taifa, uongozi wa mkoa wa Mwanza kwa
kushirikiana na ofisi yake, wameweka vituo vya kupima magonjwa katika
mipaka ya Sirari, Mutukula na uwanja wa Ndege wa Mwanza.
0 comments:
Post a Comment