SHERIA iliyopitishwa
na wakazi wa Arumeru mkoani Arusha ya kuwachapa viboko 70 hadi 120
wasichana wanaovaa nusu uchi na wavulana wanaovaa mlegezo, kuvuta bangi,
wizi, matusi na ulevi nyakati za kazi imeanza kufanya kazi baada ya
kijana Zakayo Leonard (26) kuchapwa viboko 120 kwa makosa mbalimbali
likiwemo uchafu wa kutofua nguo zake.
Kijana huyo mkazi wa Ilboru, alihukumiwa adhabu hiyo kwa kuchapwa viboko
70 akidaiwa kutenda kosa la kumshambulia baba yake mzazi
aliyetambulika kwa jina la mzee Ng’uraa na kumng’oa jino moja.
Pia alitandikwa viboko 30 kwa kosa la kumtolea maneno machafu mzee wa
kimila (Laigwanani) na baadaye alicharazwa viboko 20 kutokana na tabia
ya uchafu wa kutofua nguo zake.
Hata hivyo, mara baada ya adhabu hiyo ya viboko 120 kwa mkupuo, kijana
huyo alizimia na kushindwa kuinuka wala kutembea hali iliyolazimika
kusaidiwa kwa kubebwa na morani wa Kimasai hadi nyumbani kwake.
Adhabu hiyo ilitekelezwa hadharani mbele ya wazee wawili wa ukoo
(Laigwanani) waliokuwa wakishuhudia huku mtuhumiwa akitakiwa kutojigusa
popote wakati wa utekelezaji wa adhabu hiyo na kwamba iwapo angejishika
popote viboko hivyo alivyochapwa vingefutwa na kurejea upya.
Wazee wa makabila ya Wamasi, Waarusha na Wameru wamejiwekea utaratibu wa
kimila bila kujali kama unafuata maadili ya mwanadamu kwa kuwaadhibu
wahalifu hadharani bila kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.
0 comments:
Post a Comment