BAADA ya
kuvuja kwa picha katika mitandao ya kijamii wiki iliyopita,
iliyowaonesha askari wawili wa usalama barabarani wakiwa ‘kimahaba niue’
ndani ya sare za kazi na kusababisha kupoteza ajira zao kutokana na
kukiuka maadili, siri zaidi nzito zimezidi kuvuja kuhusiana na ishu hiyo
na Amani limemuibua afande wa kike baada ya kumsaka sana.
Kwa mujibu wa vyanzo makini kutoka wilayani Misenyi mkoani Kagera,
askari wa kike aliyeonekana kwenye picha hiyo chafu, WP. 8898 Veronica
Mdeme, inadaiwa kuwa alipata uhamisho kutoka polisi mkoani humo na
kupelekwa katika wilaya mpya ya Misenyi mwaka 2011 ambako mwaka mmoja
baadaye, ndipo akapigwa picha hiyo iliyoleta gumzo kubwa ndani na nje ya
Bongo.
Ilidaiwa kwamba, picha hiyo ilipigwa katika barabara ya lami iendayo
Mutukura, umbali wa Kilomita 50 kutoka Misenyi na kwamba askari hao
walikuwa katika Kituo cha Polisi cha Kyaka.
Nguzo ya umeme inayoonekana nyuma yao, ni zile zinazopeleka umeme nchini Uganda kutoka Bwawa la Umeme la Mtera, Tanzania.
Nguzo ya umeme inayoonekana nyuma yao, ni zile zinazopeleka umeme nchini Uganda kutoka Bwawa la Umeme la Mtera, Tanzania.
ILIKUWA PICHA YA KISHKAJI TU LAKINI…
Habari zilidai kuwa, askari hao Veronica, F.7788 Mpaji Mwasumbi na PC Fadhil Linga, walikuwa zamu moja na kwamba picha hiyo ilipigwa katika mazingira ya kishkaji tu lakini baadaye ikaja kuzua balaa kubwa.

Ilisemekana kwamba, Linga ndiye aliyewapiga picha wenzake ambao habari
zisizothibitishwa zilisema kuwa walikuwa na uhusiano wa kijamii.
Madai yalizidi kutiririshwa kwamba baada ya kupigwa kwa picha hiyo,
Linga alibaki na nakala katika kamera yake kwa muda wa miezi kadhaa
kabla ya kugundua kuwa kumbe ilikuwa ni dili.
AWAGEUZIA KIBAO
Ilidaiwa kwamba, katika hali isiyotarajiwa, Mpaji na Veronica hawakuamini masikio yao baada ya Linga kuwaambia kwamba alihitaji kupata ‘kitu kidogo’ kutoka kwao ili aweze kuendelea kuhifadhi siri ya picha hizo.

Ilisemekana kuwa afande huyo aliwaambia wawili hao kama ataivujisha picha hiyo kwenye mitandao ya kijamii, watapoteza kazi.
“Baada ya kuambiwa hivyo, jamaa walilegea kabisa. Mwanzoni walitia ngumu
lakini walipoona jamaa amekomaa, hawakuwa na jinsi zaidi ya kukubaliana
naye, hivyo akawa anapata kitu kidogo kila alipojisikia na kuwa nipe
nikupe na hakuna uhakika kama dada Vero alisalimika kwenye mambo mengine
kwani naye alikuwa akitumia nguvu kubwa kuhakikisha mumewe hajui,”
kilidai chanzo hicho.
WAAMUA KUJILIPUA, WAMSHTAKI
Ilielezwa kwamba, baada ya ‘kutolewa upepo’ kwa muda mrefu na kuonekana kama wangekuwa ATM ya kudumu ya Linga, Mpaji na Veronica waliamua kujilipua na kwenda kumshtaki kwa kigogo wa juu wa jeshi la polisi mkoani humo ambaye anatajwa kuujua mchezo mzima ulivyokuwa.

Ilisemekana kwamba, kiongozi huyo alilichukulia jambo hilo kwa uzito
wake na kuwakalisha wote watatu ili kuzungumza nao.Iliendelea kudaiwa
kuwa katika kikao kati ya askari hao na bosi wao, wawili hao walikiri
kupigwa picha hiyo na kuomba msamaha, lakini wakamlalamikia mwenzao
ambaye naye alikiri kufanya kitendo hicho, kwa kuwageuza kuwa ATM.
Ilidaiwa kuwa mkubwa huyo alimuamuru Linga kuzifuta picha hizo na
kuwataka kusameheana, kwani kitendo walichokifanya ni kibaya na
kinachoweza kuhatarisha ajira zao. Linga alikubali ‘kuzi-diliti’ picha
hizo!
WAGAWANYWA, LINGA ARUDIA
Ikazidi kudaiwa kuwa ili kuwafanya waishi kwa amani, waligawanywa katika vituo tofauti vya kazi mkoani humo huku mmoja wao, Mpaji akipelekwa Dar ambako alikwenda kusoma Chuo cha Polisi Kurasini.
Ikazidi kudaiwa kuwa ili kuwafanya waishi kwa amani, waligawanywa katika vituo tofauti vya kazi mkoani humo huku mmoja wao, Mpaji akipelekwa Dar ambako alikwenda kusoma Chuo cha Polisi Kurasini.
“Wakiwa katika vituo hivyo tofauti, Linga alitulia kwa muda mchache tu
kabla ya kuanza tena usumbufu wake, hasa kwa Veronica ambaye anadaiwa
kuwa mke wa mtu. Ni katika usumbufu huo wa mara ya pili, akina Mpaji
wakaamua kumjibu jeuri jamaa, hawakuwa na uoga tena kwa vile suala lao
lilishafahamika kwa wakubwa,” kilisema chanzo chetu.
Inaelezwa kwamba majibu ya jeuri kutoka kwa Vero na Mpaji yalimuudhi
Linga ambaye kwa lengo la kuwakomoa, aliamua kuzitupa picha hizo katika
mitandao mbalimbali ya kijamii ambako nako zilizagaa kwa kasi ya moto wa
kifuu na kuwafikia watu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na vyombo vya
habari vilivyoamua kuripoti.
“Picha hiyo ilipoonekana mtandaoni, moja kwa moja polisi walijua
imewekwa na Linga kwa sababu hakukuwa na mtu mwingine aliyefahamu kuhusu
picha hiyo. Ndiyo maana wote watatu walifukuzwa kazi siku moja,
hawakuwa na sababu ya kuhangaika kujua nani kaweka,” kilisema chanzo
hicho.
PICHA YA MREMBO YAWA GUMZO
Baada ya kufukuzwa kazi kwa wahusika hao watatu, kumekuwa na picha za mrembo mkali ambaye amekuwa akifananishwa na Veronica huku kukiwa hakuna uthibitisho wa moja kwa moja kama kweli ni yeye (angalia picha ukurasa wa mbele).

Kwa mujibu wa maoni lukuki katika mitandaoni, kama kweli mrembo huyo
ndiye huyo askari wa kike, basi jamaa aliyekuwa naye kimahaba,
alistahili adhabu yoyote kuliko kukosa mahaba hayo.
“Ni kama walivyoimba wale watoto wa Yamoto Band, yaani nzi kufia kwenye
kidonda siyo ufala bali kupenda. Huyu mtoto mashalaah,” ilisomeka sehemu
ya maoni ya stori hiyo ambayo ndiyo habari ya mjini kwa sasa.
Juzi, Amani lilimtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Henry
Mwaibambe ili kumsikia nini kinaendelea baada ya askari hao kufukuzwa
kazi lakini hakuwa hewani.
Naye msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, Advera Senzo alipopigiwa simu
na kuulizwa alisema walishafukuzwa kazi hakuna kingine lakini akaelekeza
apigiwe simu Mwaibambe.
0 comments:
Post a Comment