8:15 AM
Ipo kimtandao zaidi
Taasisi hiyo iliyoanzishwa muda mrefu ikapotea, sasa imeibuka upya na inawaliza wengi ambapo inaendesha shughuli zake kimtandao na wahusika hutumia utundu kuingilia mawasiliano katika akaunti za watu katika facebook na kuweka ushuhuda kuwa wamiliki wamefanikiwa kupata mkopo bila riba tena kwa masharti rahisi.

Mtandao umegundulikaje?
Mmoja wa wasomaji wa paparazi aliyefahamika kwa jina la Lulu, hivi karibuni alileta malalamiko yake akieleza jinsi wahusika wa utapeli huo walivyoingilia mawasiliano yake ya Facebook, wakamlisha maneno kuwa aliomba mkopo wa shilingi milioni 3 baada ya kutoa shilingi 95,000 kwa ajili ya uanachama na akapewa fasta.

Kwenye ukurasa wa Facebook wa Lulu, kulikuwa na maelezo ya kupika kuwa,
Tanzania Loan Society ni taasisi iliyo chini ya Rais Jakaya Kikwete kwa
msaada wa Rais wa Marekani Barack Obama huku watendaji wakuu wakiwa ni
Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda na Mbunge wa Chalinze, Mhe.Ridhiwani Kikwete.
Ikadaiwa eti muweka hazina wa taasisi hiyo ni Zainabu Kikwete huku namba
zake za simu zikitajwa kuwa ni 0767 602 518 na 0713 009 819, lengo la
mpango huo likiwa ni kuhakikisha Watanzania wanaondokana na umaskini kwa
kupewa mikopo kwa masharti nafuu.
Chini ya maelezo hayo kuna linki ya kuingia kwenye mtandao wa taasisi
hiyo feki (ambapo ukiufungua unakuta nembo ya serikali ya Tanzania na
maelezo yanayomshawishi mtu yeyote kuamini kuwa siyo ishu ya kitapeli.
Kinachomsukuma mtu kuingia mtegoni ni kwamba, kwanza wanahusishwa
viongozi wakubwa, pili matapeli hao wanaeleza kuwa makao makuu ya
taasisi hiyo ni Posta jijini Dar kwenye jengo la Utumishi, ghorofa ya 5,
chumba namba 30 na anayehitaji mkopo kuanzia laki moja hadi milioni 50
anatuma 95,000 kupitia namba za muweka hazina (Zainabu Kikwete feki).
Paparazi laingia kazini
Baada ya kupatikana kwa taarifa hizo, Septemba 28, mwaka huu, paparazi walianza uchunguzi kwa kuthibitisha kama namba za Zainabu zimesajiwa kwa jina gani ambapo ilionekana imesajiliwa kwa jina la Zainabu Kikwete.

Kisha paparazi alimpigia Zainabu, alipopokea na kuulizwa kuhusiana na
taasisi hiyo alisema ni kweli ipo na maelezo yote yapo kwenye mtandao
wao huku akimsisitiza paparazi kutuma pesa ili atumiwe mkopo.
paparazi watinga Jengo la Utumishi
Baada ya kujiridhisha, paparazi wetu walimpigia tena Zainabu na kumtaarifu kuwa wapo njiani kuelekea ofisini kwao, kwa kujiamini alisema hakuna shida na kama ni mkopo upo unawasubiria.

Baada ya paparazi wetu kufika kwenye jengo la Utumishi, walimpigia tena
simu Zainabu kumjulisha kuwa wameshafika ambapo alidai wametoka kidogo
ofisini (eti wameenda kukusanya madeni sugu) na kwamba wakutane kesho
yake.
Paparazi wetu wakiwa nje ya jengo hilo, waliongea na mmoja wa walinzi na
kumuuliza juu ya uwepo wa taasisi hiyo ambapo alieleza kuwa, haipo na
wengi wamekuwa wakifika hapo baada ya kutapeliwa.
Ili kupata taarifa rasmi, paparazi walifika kwenye ofisi ya mmoja wa
maafisa habari wa Ofisi ya Rais, Menejimenti na Utumishi wa Umma,
Florence Laurence ambaye alikiri taasisi hiyo ya kitapeli kuhusisha
jengo lao na walishatoa tahadhari kwa wananchi.
Msako wafanyika
Licha ya majibu yaliyotolewa na afisa habari huyo, paparazi wetu walifika katika Ofisi ya Polisi, Kanda Maalum ya Dar, Kitengo cha Intelijensi na kutoa taarifa ambapo walichukua taarifa kuhusiana na mtandao huo na kuahidi kudili nao.

Septemba 30, mwaka huu ofisi hiyo ilitoa polisi wawili ambao
waliongozana na paparazi mpaka katika jengo la Utumishi na mhusika
alipopigiwa simu alidai siku hiyo pia walikuwa bize kukusanya madeni
sugu na kwamba waende tena kesho yake.
Kutokana na kuchengachenga kwa wahusika, polisi walishauri waachwe
wafanye kazi yao na kwamba kwa mbinu zao za kiintelijensia watawanasa
wahusika. Uchunguzi wa paparazi umebaini kuwa, mtandao huu umewaliza
wengi hivyo ni vyema watu wakawa makini.
NMB NOA WATOA ONYO LAO
Notice to our customers and the general public
NMB Management wishes to inform the public that it has come to our
attention that a body identifying itself as Tanzania Loans Society is
claiming to be affiliated with NMB and has issued a statement on its
website http://www.tanzanialoans.wapka.mobi/ , claiming to issue loans
financed by NMB through NMB Branch Managers.
Moreover, the Tanzania Loan Society has also indicated that the loan
application forms and registration fee proceeds can be remitted through a
mobile phone number.
NMB Management wishes to inform our customers and the general public
that we do not have any business affiliation with this society. NMB only
issues loans through branches and under no circumstances are
application fees or loans remitted through mobile phones.
Customers and the general public are hereby cautioned not to engage with
this society on any transaction involving NMB Plc and the bank shall
not be held responsible for any transaction or agreement transacted with
the Tanzania Loans Society.
About NMB:
NMB Plc is the leading bank in Tanzania, with over 145 branches, 1.7
million customers and over 500 ATM's. NMB pioneered major innovations in
the Tanzanian market including mobile banking and Pesa Fasta, a ATM
based remittance product targeted at the unbanked. NMB is also making
inroads in Corporate Banking, Treasury, and Transactional Services such
as corporate payments, collections and trade finance. NMB plays an
important role in the agricultural value chain and pioneered warehouse
receipt financing for the country's Amcos. We also support the
Government of Tanzania through all our branches of which 60% are in
rural areas.
Ridhiwani Kikwete akana kuhusika na Tanzania Loan Society, atahadharisha kuwa ni matapeli
Hii ni taarifa ya Ridhiwan Kikwete aliyoiandika kupitia Facebook
kuhusiana na kuhusishwa na mradi uitwao Tanzania Loan Society ambao
anadai umekuwa ukitumia jina lake na la Waziri Mkuu Mizengo Pinda
kutapeli wananchi.
Habari zenu, mabibi na mabwana, marafiki zangu wa kwenye mtandao na wale wasio marafiki zangu ambao naamini kwa namna moja au nyengine mtakapo soma habari hii mtaipeleka kwa jamaii inayowazunguka ili kuweka hali vizuri .
Maisha ni kuhangaika na kwamba inataka mtu anayefahamu njia sahihi kuweza kujua kuwa nikitumia njia hii hali itakuwa sawa na pengine mambo yangu yatanyooka.hii inaweza kuwa ndiyo maana halisi ya hangaika ufanikiwe. lakini tafsiri hii haiwezi kuwa kutumia njia za kudhulumu, kukaba, kuiba au kufanya utapeli ili ufanikishe malengo yako mabaya dhidi ya mtu au kikundi fulani cha watu.
Hivi karibuni nimekuwa napokea sana emails, sms, na hata tweets juu ya kitu kinachoitwa TANZANIA LOAN SOCIETY, ambacho kwa namna moja au nyengine kinaonekana kuwa ni mradi ambao umeanzia katika mikono ya Raisi Barack Obama kuja Tanzania kupitia Raisi Dr. Jakaya Kikwete na sasa mie nikishirikiana na Waziri Mkuu Bwana Mizengo Kayanza Pinda tunauendesha.Jambo ambalo si la ukweli hata kidogo na naomba tumia nafasi hii kulikanusha kabisa mbele ya umma wa watanzania na wale wote ambao kwa namna moja au nyengine wanafuatilia ninavyotuma kwenye kurasa hii.
Kwa masikitiko makubwa sana napenda kuweka hadharani kuwa JAMBO HILI SI LA KWELI na kwamba HAKUNA KITU na kwa yeyote ambaye atakuwa ametoa hela yake basi atakuwa AMETAPELIWA.
Kwa upande wangu niwaombe ndugu zangu na vijana wenzangu watanzania kuwa makini sana na mambo haya ya mitandao. maana wanaotangaza vitu kama hivi wanaweza kuwa na nia mbalimbali ikiwemo, KUTUMIA JINA LANGU ILI KUWAIBIA WATU, lakini pia KUTUMIA JINA LANGU ILI KUNICHAFUA, au kutumia NJIA HII IIKIWA NI SEHEMU YA KUJIPATIA KIPATO KISICHO HALALI.
Hivyo ni ushauri wangu kwenu vijana wenzangu ambao ninaamini kuwa muliamini kuwa jambo hili ni ukweli kuacha kuamini vitu mnavyoviona pasi kuwa na taarifa za uwakika.tuwe wepesi wa kuuliza kabla hatujajaribu maana VYENGINE NI SUMU NA HAVIONJEKI.
Nimalize kwa kuwashukuru wote ambao kwa namna moja au nyengine wamekuwa wakinipigia simu kunijulisha na hata wale walioandika ujumbe mfupi wa maneno pia. pia kuwapa pole wote ambao kwa namna moja au nyengine wameathiriwa na zoezi hili. lakini haukuwa nia yangu kuona dhuruma hii ikitokea ila ni ukweli kuwa lazima uelewe vizuri kuwa uchunguzi wa kina lazima ufanyike na kujiridhisha pasipo kukurupuka maana unaweza fanya jambo kumbe ndiyo unalikuza. lakini pia niwaombe wale ambao kwa namna moja au nyengine kurasa zao za face book zimetumika kurusha matangazo haya ya kiutapeli waone jinsi gani wanaweza kulizungumzia jambo hili ili kuwasaidia wengi ambao wameathirika na imani yao juu ya hili.
MIMI NDUGU YENU
RIDHIWANI JAKAYA KIKWETE
AKSANTENI KWA KUSOMA TAARIFA HII.

0 comments:
Post a Comment