ASKARI
wa Kikosi cha Usalama Barabarani waliopiga picha ya mahaba wakibusiana
huku wakiwa wamevaa sare za Jeshi la Polisi na picha yao ikasambaa
katika mitandao mbalimbali ya kijamii wamefukuzwa kazi.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kagera, Henry Mwaibambe amethibitisha leo kwa
waandishi wa habari mkoani humo kuwa, askari hao na mwenzao aliyewapiga
picha wametambuliwa na tayari wamefukuzwa kazi kwa kitendo hicho cha
kulidhalilisha Jeshi la Polisi.
Kamanda
Mwaibambe amewataja askari hao kuwa ni PC Asuma Mpaji Mwasumbi mwenye
namba F.7788, PC Fadhiri Linga mwenye namba G 2122 na PC Veronica
Nazaremo Mdeme, wote walikuwa askari wa kikosi cha usalama barabarani
wilayani Misenyi, mkoani Kagera.
0 comments:
Post a Comment