TAARIFA za Ujumbe unaosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Mama
Maria Nyerere kafariki SI SAHIHI.
Ndugu wa Karibu wa Mama Maria amekanusha taarifa hizo kwa kuandika hivi katika akaunti yake ya Facebook::
Bwana asifiwe. Tunamshukuru Mungu kwa afya na uzima wa Mama Maria Nyerere ambao Mungu amemjaalia mpaka saa hii ninapoandika kwenye facebook. Mungu aendelee kukupa maisha marefu na afya njema na hofu ya Mungu ikakutawale kwa maana umemtegemea sana yeye siku zote. Nakemea kila roho ya uzushi na matamshi yasiofaa kwa Mama yetu. Nayarudisha yalikotoka kwa mamlaka ya Yesu wa Nazareti. Mabaya hayatamkuta bali ulinzi wa Bwana utamzunguka Mama yetu na ataishi akifurahia ukuu wa Bwana Yesu sawa na neno la Mungu toka Zaburi 91:16. Praise God.
0 comments:
Post a Comment