MNENGUAJI wa Kundi la Kanga Moko, Zawia Hamis ambaye usiku wa Jumatano iliyopita alipigwa risasi mbili mwilini na mtu aliyedaiwa ni askari polisi, ameweka undani wa sakata hilo.
Mnenguaji wa Kundi la Kanga Moko, Zawia Hamis akionyesha sehemu
alikopigwa risasi mbili mwilini na mtu aliyedaiwa ni askari polisi.
alikopigwa risasi mbili mwilini na mtu aliyedaiwa ni askari polisi.
Akizungumza na gazeti hili juzi nyumbani kwake Mwananyamala jijini Dar,
majeruhi huyo alisema tukio hilo lilijiri maeneo ya Mwananyamala-
Kisiwani karibu na Ofisi za Chama cha Wananchi (Cuf) na kuongeza kuwa,
kisa ni kubishana na askari huyo aliyetaka kuzimwa kwa matarumbeta
kutoka kwenye kikundi chao kilichokuwa kikipita eneo hilo.
“Sisi tulikuwa tukipita na matarumbeta, askari wakatusimamisha na
kutuamuru tuyazime kisha kutaka kutukamata watupeleke kituoni eti
serikali imekataza.
“Tuliwaambia mbona ni mapema sana kwani ilikuwa saa kumi alasiri na Kova
alisema ngoma za Kanga Moko, Kigodoro na nyingine zisipigwe usiku. Pia
tuliwaambia tulichokuwa tukikifanya si ngoma hasa, ni matarumbeta
tunapita kuwaalika watu kuwa leo kuna shughuli sehemu.
“Baada ya majibu hayo ndipo askari mmoja hakutaka hata kuendelea na
mazungumzo, alitoa bastola kiunoni na kunipiga risasi mbili, moja
kiunoni, nyingine kwenye mbavu halafu akapiga tena hovyo hewani risasi
zilizobaki. Kwa kweli nimeumia sana,” alisema Zawia.
Mnenguaji huyo alisema kutokana na hali yake kuwa mbaya alipelekwa Kituo
cha Polisi cha Mwinjuma na kupewa Polisi Fomu No. 3 (PF3) kisha
kukimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kinondoni, Mwananyamala kwa
ajili ya matibabu ambapo kwa mujibu wake alitolewa risasi mbili.
Baada ya kuzungumza na majeruhi huyo, waandishi wetu walikwenda kwenye Kituo cha Polisi Mwinjuma ambako ndiko alikoripoti PF3.
Baada ya kuzungumza na majeruhi huyo, waandishi wetu walikwenda kwenye Kituo cha Polisi Mwinjuma ambako ndiko alikoripoti PF3.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Dar, Camillius Wambura hakupatikana
kwa simu juzi kuzungumzia tukio hilo lakini gazeti hili linaendelea
kufuatilia.
0 comments:
Post a Comment