Sakata la mastaa wakiwemo Wema Sepetu na
Nasibu Abdul ‘Diamond’ kupiga picha chafu kisha kuzitundika mitandaoni
limetinga bungeni baada ya juzikati baadhi ya wabunge kulishupalia.
Hilo liliibuka Suzi mjengoni katika
kipindi cha maswali na majibu ambapo Mbunge wa Jimbo la Mchinga, Saidi
Mtanda alitaka kujua hatua zilizochukuliwa na serikali katika
kukabiliana na tabia za watu maarufu kupiga picha zisizo na maadili
kisha kuziweka mtandaoni.
Katika kujibu swali hilo, Naibu Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia alisema:
“Tunajitahidi kuhakikisha wanaofanya hivyo wanachukuliwa hatua stahili
ili kukabiliana na matendo hayo ambayo ni kinyume na maadili.”
Katika kuonesha kutoridhika na majibu ya
waziri, Mheshimiwa Mtanda alipopewa nafasi aulize swali la nyongeza
alisema: “Mheshimwa spika nahisi swali langu halijajibiwa ipasavyo.
Nilichotaka kujua ni hatua ambazo zimechukuliwa kwa baadhi ya watu
mastaa kama vile Wema na Diamond ambao hupiga picha zao zisizofaa kisha
kuziweka mtandaoni.”
Kufuatia swali hilo, Nkamia alisimama na
kujibu kwamba, serikali imeweka mikakati na njia sahihi za kukabiliana
na tabia hiyo na kwamba wale ambao watabainika watachukuliwa hatua
zinazostahili.

“Mheshimiwa kuhusu hizi picha za juzi
zilizosambaa mtandaoni, tunazifuatilia kujua zimeanzia wapi na taarifa
zake zikoje kwani hata mimi bado sijaziona ila tutachukua hatua
tutakapobaini zilikotokea.”
0 comments:
Post a Comment