

Mshambuliaji wa Liverpool anaweza kwenda Barcelona kwa dau la puandi milioni 80.


Siku za furaha: : Suarez akishangilia kushinda kiatu cha dhahabu pamoja na mtoto wake Delfina na mke wake Sofia

Liverpool wameanza mbio za kumuwania mchezaji wa Benfica, Lazar Markovic.
Mserbia, Markovic ni moja ya wachezaji bora wenye umri mdogo katika soka la Ulaya na bei yake ni paundi milioni 20.
Japokuwa
Liverpool walikuwa wanaweka ngumu kwa dau hilo, lakini baada ya kupokea
taarifa za FIFA kuhusu kumfungia Suarez wamelazimika kukubali na
kumruhusu Muurguay huyo kuondoka klabuni hapo.
Licha
ya kufungiwa, Liverool wanaamini Barcelona inaweza kulipa paundi
milioni 80 na tayari mmiliki mkuu wa klabu hiyo John W Henry anaonekana
kutokuwa tayari kumuuza kwa bei rahisi.
Mwanasheria
wa Suarez Alejandro Balbi alikuwa Barcelona kujadili hatima ya mteja
wake, wakati kocha mpya wa Barca Luis Enrique alisema hakuna tatizo
lolote juu ya kumsajili nyota huyo mwenye miaka 27.
Alimfananisha
Suarez na mshambuliaji gwiji wa Barca Hristo Stoichkov na alisema :
‘Stoichkov kiukweli aliwahi kufanya madhambi makubwa dhidi ya mwamuzi,
lakini aliendelea kufirika kuwa mcheza mkubwa".
Kama
Liverpool watamuuza Suarez kwa paundi milioni 80, hiyo itakuwa biashara
nzuri kwa Brendan Rodgers ambapo atatumia mkwanja huo kuimarisha kikosi
chake.
0 comments:
Post a Comment