Vuguvugu
la Sunni lenye msimamo mkali la ISIS ambalo limeteka maeneo ya
Kaskazini
mwa Iraq limesambaza picha ambazo zinaonyesha jinsi wapiganaji wake
walivyoangamiza idadi kubwa ya wanajeshi wa Iraq.
Kwa
mujibu wa BBC, Picha zinazosambazwa kupitia internet zinaonyesha miili
ya watu iliyosongamana ndani ya mtaro ikiwa imepelekwa hapo kwa kutumia
malori.
Wapiganaji wa ISIS wanaonekana wakibeba bendera nyeusi ya huku wakichoma miili hiyo na kulazimisha mateka kulala chini.
Wakati
huo huo, Serikali ya Marekani inafikiria kuingia katika mazungumzo ya
moja kwa moja na Iran juu ya hali ya usalama huko Iraq.
0 comments:
Post a Comment