INASIKITISHA sana!
Denti mmoja wa kike wa darasa la saba anayesoma katika Shule ya Msingi
Chanzige B iliyopo Kisarawe, Pwani amejikuta katika wakati mgumu baada
ya kulawitiwa na kusababishiwa maumivu makali sehemu zake za siri.
Simulizi ya binti huyo inayouma sana,
inaeleza kuwa denti huyo alifanyiwa unyama huo
na vijana watatu ambao bado hawajafahamika majina yao mara moja lakini amekuwa akimtaja mmoja kwa jina la Musa.
Tukio hilo lenye sura ya majonzi hasa kwa wazazi na watoto, lilitokea hivi karibuni Kisarawe mkoani Pwani lakini ilifanywa siri kwa muda mrefu na mtoto huyo kukaa bila matibabu.

Chanzo chetu cha habari kinasema kuwa,
shangazi wa mtoto huyo ambaye anaishi naye ndiye sababu ya kutopata
tiba, kwani anadaiwa kuchukua kiasi cha shilingi 200,000 kutoka Musa
anayetajwa kuwa mmoja wa wahusika kama kifunga mdomo.
Denti wa kike wa darasa la saba
anayesoma katika Shule ya Msingi Chanzige B iliyopo Kisarawe, Pwani
aliyefanyiwa unyama wa kulawitiwa na vijana watatu.
Chanzo hicho kikazidi kusema kuwa, awali
kesi hiyo ilifikishwa katika Kituo cha Polisi Kisarawe na kufunguliwa
jalada lakini shangazi wa mtoto huyo aliamua kuyamaliza mambo hayo na
mmoja wa watuhumiwa baada ya kupewa kiasi hicho cha fedha.
Uchunguzi wa Amani umegundua kuwa,
sakata hilo liliripotiwa katika Kituo cha Polisi Kisarawe na kufunguliwa
jalada nambari KIS/RB/326/2014, ambapo Fomu ya Polisi Nambari 3 (PF3)
ilitolewa kwa ajili ya matibabu ya mtoto huyo.
Akisimulia zaidi, mama mzazi wa mwanafunzi aitwaye Mariam Said alisema, alipata taarifa za mwanaye kukumbwa na masahibu hayo ambapo aliamua kusafiri kutoka Mlandizi anapoishi hadi Kisarawe kufuatilia tukio hilo.

Binti huyo alisema alifanyiwa ukatili
huo wakati akitokea shuleni na kwamba alimweleza shangazi yake kila kitu
kuhusiana na tukio hilo kabla ya kwenda naye polisi kutoa taarifa.
“Baada ya hapo tulikwenda katika
Hospitali ya Kisarawe lakini sikupata matibabu kwa sababu shangazi
alisema hana pesa ya malipo, kukarudi nyumbani na kununua dawa kwenye
maduka ya dawa,’’ alisema mtoto huyo na kuongeza:
“Pale hospitalini, shangazi alitakiwa kutoa kadi ya Bima au shilingi 10,000 ili nitibiwe. Sasa hakuwa na Bima wala hiyo pesa ndiyo maana ikashindikana.”
“Pale hospitalini, shangazi alitakiwa kutoa kadi ya Bima au shilingi 10,000 ili nitibiwe. Sasa hakuwa na Bima wala hiyo pesa ndiyo maana ikashindikana.”
Gazeti hili lilifunga safari hadi Shule
ya Msingi Chanzige B na kuzungumza na Mwalimu Mkuu, Issac Eliah ambaye
alikiri kupokea taarifa ya mwanafunzi wake kubakwa na kulawitiwa kutoka
kwa shangazi wa mtoto huyo na kutoa ruhusa kwa ajili ya matibabu.
Shangazi wa mtoto huyo alipotakiwa
kuzungumzia ishu ya kuzima kesi hiyo kwa madai ya kupewa shilingi
200,000 alisema: “Mimi sitaki kuzungumzia suala hilo, nendeni polisi
mkaulize siyo kuniuliza mimi.”
0 comments:
Post a Comment