Tuesday 28 October 2014

Tanzania Yakataa Rasmi Mambo ya Ndoa za Mashoga na Wasagaji




SERIKALI ya Tanzania imekataa rasmi kutambua ndoa za jinsia moja (ushoga) kama
moja ya agenda za maendeleo katika malengo ya milenia 2015 mpaka 2030 katika mkutano wa Umoja wa Mataifa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam kwenye mkutano wa majadiliano ya malengo ya milenia yanayotazamiwa kumalizika mwakani na kuanza malengo mapya, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy amesema serikali ya Tanzania imekataa kutambua ushoga kama moja ya agenda za maendeleo.
“Tunatambua haki za binadamu, usawa wa kijinsia kati ya wanaume na wanawake na hata katiba yetu pendekezwa imetoa haki za sawa kati ya wanaume na wanawake lakini katika swala la kutambua ndoa za jinsia moja hilo tumekataa,” amesema Balozi Mushy
Amesema kwamba tumewaambia nchi zilizoendelea na wahisani wa maendeleo katika Umoja wa Mataifa kwamba swala la ndoa za jinsia moja (ushoga) si agenda ya watanzania na si agenda ya maendeleo.

Balozi Mushy aliongeza kwamba serikali ya Tanzania imeweka msimamo huo zaidi hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete aliagiza hivyo kwa maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje pamoja na Waziri husika kukataa shinikizo la kukubali swala ushoga kama agenda za maendeleo.
MASHOGA
Amesema kwamba watanzania wanataka maswala yanayowagusa kama vile maji, elimu, huduma bora za afya, miundombinu ya umeme, ajira, umaskini na kuondoa umaskini wa kipato.
Balozi Mushy alifafanua zaidi kwamba mambo ya ushoga na ndoa za jinsia yanakwenda kinyume na maadili ya watanzania, maisha, historia, utamaduni, mila na desturi za mtanzania sinakataza maswala ya ushoga.

Amesema kwamba serikali inatambua kwamba sheria ya mwenendo wa makosa ya kujamiiana yaliwekwa na mkoloni mwingereza kabla ya uhuru na serikali ya Tanganyika imerithi kutoka kwenye serikali ya mwingereza.

0 comments:

Post a Comment