Wakati rafiki yake kipenzi, Wema
Sepetu akidaiwa kunasa mimba ya Diamond , Aunt Ezekiel yeye
amesema bado hajaona mwanaume anayeweza kumtia mimba na
hatimaye kuitwa baba wa watoto wake.
Akipiga stori na mwanahabari wetu ,
Aunt Ezekiel amedai kuwa kuna wakati unaweza kumuona yupo
kwenye ndoa au uchumba lakini haimaanishi kuwa kuwepo katika
mazingira hayo ndo anaweza kuzaa au kushika mimba kwani suala
hilo kwake ni kubwa sana na hajafikiria kama linaweza kutokea
kwa sasa…
“Siyo kwamba sina uwezo wa kubeba mimba, hapana, suala kubwa hapa ni kwamba bado sijaona mwanaume wa kunizalisha.
“Ni kweli nilikuwa kwenye
ndoa lakini sikutaka kubeba mimba na ndo maana hadi sasa
hivi nipo kama ninavyoonekana,” alisema Aunt Ezekiel.
0 comments:
Post a Comment