KABANG! Baada
ya kutoonekana katika pozi za kimahaba kwa muda mrefu, kwa mara ya
kwanza, staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe ‘Gambe’
amenaswa ‘live’ na mwanaume anayedaiwa kuwa ni mume wa mtu, Risasi
Jumamosi limesheheni.
Kwa muda mrefu Wolper amekuwa makini na
picha zake za kimahaba tangu alipokuwa akitoka kimapenzi na
mfanyabiashara maarufu jijini Dar, Abdallah Mtoro ‘Dallas’.
CHANZO CHAMWAGA MTONYO
Awali, chanzo makini kilipenyeza habari kuwa kuna mawasiliano yamenaswa ‘kimafia’ ambayo yalitoka kwa Wolper kwenda kwa rafiki yake yakionesha anabanjuka na mwanaume huyo wa mtu aliyejulikana kwa jina moja la Gee.

YADAIWA NI MUME WA SHOSTI YAKE
Chanzo hicho kilikwenda mbali zaidi kwa kudai kwamba licha ya kuwa ni mume wa mtu, mwanaume huyo ni bwana wa rafiki yake kutokana na mawasiliano hayo yalivyosomeka.
Chanzo hicho kilikwenda mbali zaidi kwa kudai kwamba licha ya kuwa ni mume wa mtu, mwanaume huyo ni bwana wa rafiki yake kutokana na mawasiliano hayo yalivyosomeka.
“Mashabiki kila siku huwa wanamtetea
Wolper na skendo zake, sasa nakutumia picha pamoja na ‘chating’ zake
alizokuwa akichati na shoga yake kuhusiana na jamaa huyo,” kilisema
chanzo hicho.
PICHA ZATUA RISASI JUMAMOSI
Baada ya kuzinyaka habari hizo, mwanahabari wa Risasi Jumamosi alimtafuta sosi huyo na kufanikiwa kuzitia kibindoni picha hizo kisha kazi ya kuwasaka wahusika ikaanza.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, mwanahabari wa Risasi Jumamosi alimtafuta sosi huyo na kufanikiwa kuzitia kibindoni picha hizo kisha kazi ya kuwasaka wahusika ikaanza.
Wa kwanza kutafutwa alikuwa ni Gee
ambaye kwa mujibu wa vyazo tofauti, ilidaiwa kuwa kwa sasa hayupo Bongo
na hakuacha mawasiliano yoyote tangu alipoondoka.
Baada ya jitihada za kumsaka mwanaume huyo kugonga mwamba, paparazi wetu alimtwangia simu Wolper ambaye alieleza kila kitu:
Paparazi: Mambo vipi Wolper, nasikia makelele unaweza kusogea sehemu yenye utulivu kuna ishu nataka tuongee?
Wolper: Niko msibani na sasa hivi ndiyo zoezi la kuaga mwili, ngoja niingie kwenye gari nikupigie.
Baada ya dakika 45
Baada ya dakika 45
Wolper: Haya niambie wangu niko sehemu nzuri.
Paparazi: Ni hivi, kuna habari imetufikia ikiambatanishwa na picha na baadhi ya chating inakuhusu wewe!
Wolper: Habari gani hiyo mbona unanitisha?
Paparazi: Ni hivi, kuna habari imetufikia ikiambatanishwa na picha na baadhi ya chating inakuhusu wewe!
Wolper: Habari gani hiyo mbona unanitisha?
Paparazi: Kuna
picha zinakuonesha wewe ukiwa katika pozi la kimalavidavi na jamaa
anayedaiwa kuwa ni mume wa mtu. Ukiachana na picha hizo,
zimeambatanishwa chating zinazoonesha ulikuwa ukichati na rafiki yako
kumueleza kuwa mwanaume uliye naye ni mume wa mtu!
Wolper: Kiukweli
kabisa bila ya hata kupepesa macho hizo picha ni zangu na zimepigwa kwa
kutumia simu yangu tangu mwaka juzi lakini kuhusiana na hizo chating
siyo zangu hata wewe unaweza kuwa shahidi kwani mara nyingi huwa
tunachati na unajua vizuri ‘floo’ yangu katika kuandika SMS.
Wolper: Hapana, huyo ni mshikaji wangu tu na tulipiga picha hizo tukiwa baa tena kipindi kile nahamia tu Mwananyamala (Dar) na sasa hivi hata sijui huyo mshikaji yuko wapi.
Paparazi: Ina maana huna mawasiliano naye kwa muda mrefu, mtu ambaye mlipiga naye picha kimahaba namna hii?
Wolper: Kweli kabisa, sina mawasiliano naye kitambo nikimaliza tu kuongea na wewe nitamtafuta na kumuuliza kulikoni picha hizo kuvuja.
Paparazi: Si ulisema umepiga katika simu yako wewe si ndiyo wa kujiuliza kwa nini picha zimevuja?
Wolper: Nilimzawadia simu kama rafiki yangu na picha zikiwa humohumo sikuzifuta.
Wolper: Nilimzawadia simu kama rafiki yangu na picha zikiwa humohumo sikuzifuta.
Paparazi: Haya Wolper ngoja nikuache mi niendelee na majukumu.
Wolper: Poa wangu baadaye nitakucheki.
WOLPER HUYUHUYU
Hii ni mara ya pili kwa Wolper kutuhumiwa kukwapua bwana wa rafiki yake. Hivi karibuni mshiriki wa Miss Tanzania 2012, Husna Maulid alilalamika kuwa Wolper kamchukulia bwana’ke aliyemtaja kwa jina moja la Rajab, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Si Wolper pekee, ‘trendi’ inaonesha kuwa
mastaa wengi wa kike hasa wa filamu wamefanya ishu ya kuporana wanaume
kuwa sehemu ya utamaduni katika tasnia hiyo bila kujua wanajiondolea
heshima mbele ya jamii.
0 comments:
Post a Comment