Saturday, 26 July 2014

NEWS!! MWIMBAJI WA INJILI, BAHATI BUKUKU APATA AJALI


Muimbaji wa nyimbo za Injili, Bahati Bukuku.

Muimbaji wa nyimbo za Injili, Bahati Bukuku amepata ajali ya gari akiwa na dereva wake, Eddy maeneo ya Kongwa Dodoma usiku wa kuamkia leo.

Akiongea kwa simu Bahati amesema: “Ni Mungu tu aliyetuokoa, tulikuwa tunaelekea Kahama kwenye huduma ghafla tukagongana uso kwa uso na lori, gari yetu aina ya Toyota Nadia  iliruka na kubiringika kama mara tatu hivi, tumetoka tukiwa tumeumia sana.

“Hapa siwezi kusimama wala kukaa na dereva wangu kaumia sana mguu. Gari yangu imeumia sana wala huwezi kuamini kama kuna mtu katoka salama.”


Taratibu za kumhamishia Bahati kutoka Hospitali ya Kongwa kuja Muhimbili zinafanywa na ndugu pamoja na marafiki.

Tunakuombea upone haraka Bahati.

0 comments:

Post a Comment