Saturday, 26 July 2014

MWANAMKE ALIYECHOMWA MOTO SEHEMU ZA SIRI AFUNGUKA NA KUSEMA HATORUDI KWA MUMEWE JAPO ANAUJAUZITO.





Agnes Marwa akiwa amelala kwenye kitanda katika kituo cha Afya Sungusungu


Agnes Marwa (18 ) mkazi wa kijiji cha Mrito,Tarime Mara amesema kutokana na ukatili aliofanyiwa na mumewe hayuko tayari kurudi kwa mwanamme huyo ingawa ni mwaka mmoja sasa tangu waoane na kuwa na ujauzito wa mwezi mmoja na nusu.



Marwa Chacha anatuhumiwa kumpiga,kumfunga kamba na kumweka nje wakati mvua inanyesha ,kisha akaenda

jikoni na kuchukua kijinga cha moto na kuanza kumuunguza sehemu zake za siri baada ya kukuta shilingi 2000 kwenye pochi yake na kumtuhumu kuwa amepewa fedha hizo na wanaume julai 13 mwaka huu.



Baada ya kitendo hicho mtuhumiwa alitoroka na Agnes kwa mila za kikurya alificha tukio hilo hadi julai 17 mwaka huu ndipo akapelekwa katika kituo cha afya cha Sungusungu kilichopo Nyamongo.





 Mganga mfawidhi wa kituo cha afya Sungusungu Kagumilwa Kaijage amesema kuwa siku aliyofikishwa kituoni hapo alikuwa na hali mbaya kwani alikuwa akitokwa usaa katika sehemu zake za  na mapajani kutokana na kuunguzwa sehemu hizo. 





Jeshi la Polisi kanda maalum ya Rorya limesema mtuhumiwa pamoja na mama yake wametoroka na hii ni baada ya kutoa taarifa,hata hivyo jeshi hilo bado linaendelea kufanya utafiti ili liweze kumkamata mtuhumiwa.

0 comments:

Post a Comment