Friday, 29 August 2014

BREAKING NEWS: WATU 10 WAFARIKI DUNIA KATIKA AJALI HUKO MBEYA!



Watu kumi wakiwemo watoto wawili, 
wamefariki dunia papo hapo na wengine 
saba wamejeruhiwa vibaya katika ajali 
iliyohusisha magari mawili.

Ajali hiyo imehusisha gari ndogo ya abiria 
maarufu daladala lenye namba za usajili T 
237 BFB aina Toyota Hiace na gari kubwa 
aina ya Fuso lenye namba za usajili T 158 
CSV.


Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo 
wamemwambia paparazihuru kuwa ajali hiyo imetokea maeneo ya Mbalizi baada ya Hiace iliyokuwa ikitokea 
Mbeya mjini kuelekea Mbalizi kulivaa Fuso 
ilikuwa ikiingia barabarani.

Hata hivyo majina ya majeruhi na marehemu 
hayajaweza kupatikana mara moja kutokana 
na kuwa katika hali mbaya ambapo Dereva 
wa Fuso akitokomea mara baada ya tukio.


R.I.P All na pole sana kwa familia

0 comments:

Post a Comment