Thursday, 28 August 2014

MAN UTD WAKUBALIANA MKATABA WA MIAKA MITANO NA ARTURO VIDAL


MANCHESTER UNITED wamekubaliana masuala binafsi na Arturo Vidal na atasaini mkataba wa miaka mitano, lakini bado wapo katika majadiliano na klabu yake ya Juventus kuhusu ada ya uwamisho.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Chile anajiandaa   kuondoka Turin majira ya joto, na United wako katika nafasi nzuri ya kumsajili kabla dirisha la usajili halijafungwa siku ya Jumatatu jioni.



Louis Van Gaal tayari amesha kamilisha dili la nyota wa Real Madrid Angel

Di Maria, kwa kulipa kiasi cha pauni milioni  59.7 ili kupata sahihi yake, na kwa mujibu wa ripoti za Italia na Hispania, Muholanzi huyo imefikia makubaliano na Vidal kuhusu mkataba wa  muda mrefu wenye thamani ya pauni  182,000 Kwa wiki.

Hata hivyo, Juventus wapo tayari kukubali dau la United ambalo linaaminika kuwa pauni milioni 34.



Wakala wa Arturo Vidal - Fernando Felicevich jana alitua jijini Manchester kujadili masuala binafsi kuhusu kiungo huyo, Vidal anatarajiwa kuwaaga wachezaji wenzake wa Juventus kabla ya kuhamia Manchester United.

Bosi mpya wa Juventus Massimo Allegri pia amevutiwa na Javier Hernandez, na  Mmexico huyo anaweza kuwa sehemu ya dili hilo ili kufanikisha kusajiliwa kwa Vidal.

0 comments:

Post a Comment