Tumekwisha! Kikosi
maalum cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) cha Global Publishers,
kimemnasa msaidizi wa kazi za ndani (hausigeli) akifanya biashara haramu
ya kuuza mwili kwa kisingizio cha mshahara kiduchu.
Tukio hilo la aina yake liliingia kwenye kamera za OFM maeneo ya Sinza
jijini Dar, mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo msichana huyo wa kazi
alikutwa kwenye harakati za kusaka wanaume ili kuwapa penzi kwa malipo.
Mara baada ya kumnasa na kumlamba picha akiwa na wenzake ambao nao kama
yeye walikuwa wamevaa nguo fupi yaani nusu utupu, alianza kuangua kilio
hasa alipokuwa akihojiwa kwa nini anajihusisha na biashara hiyo
hatarishi katika maisha yake.
“Jamani mmenipiga picha mtanipotezea kazi yangu, jamani mimi
nimeajiriwa, ni mfanyakazi wa ndani kwa mheshimiwa Mikocheni (Dar),
nafanya kazi za ndani hii yote ni kujitafutia riziki nje ya kazi,”
alilalama binti huyo aliyekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 20 hadi
23.
Binti huyo aliwaambia OFM kwamba alifikia hatua hiyo ya kujiingiza
katika biashara hiyo ya ngono kutokana na ugumu wa maisha huku lawama
akizielekeza kwenye mshahara kidogo wa kazi za ndani.
“Mshahara wangu ni mdogo sana, nalipwa shilingi elfu 50 kwa mwezi, nina watoto wawili kijijini hivyo hautoshi. Kama vipi nitafutieni kazi nitaacha kuuza mwili,” alisema.
“Mshahara wangu ni mdogo sana, nalipwa shilingi elfu 50 kwa mwezi, nina watoto wawili kijijini hivyo hautoshi. Kama vipi nitafutieni kazi nitaacha kuuza mwili,” alisema.
Alipoulizwa namna anavyotoka kwa bosi wake kwenda kujiuza, hausigeli
huyo alisema kwamba huwa anakula dili na walinzi wa bosi wake usiku
wakiwa wamelala anatoka na akirudi freshi anawakatia walinzi chao.
Alisema kuwa yeye analala katika vyumba vya uani kwa hiyo anapotoka
waajiri wake hao inakuwa vigumu kumsikia kwani wanakuwa wamepitiwa na
usingizi.
Aliendelea kueleza kwamba kuna siku nyingine huwa anarudi nyumbani akiwa amevuna fedha nyingi kuliko mshahara wake.
“Hii kazi yangu inaniingizia kipato kikubwa sana kuliko mshahara,” alisema hausigeli huyo
0 comments:
Post a Comment