Monday, 6 October 2014

BALAA, NABII JEREMIAH ATANGAZA KIAMA,AWATAKA WAGANGA WA KIENYEJI WAJISALIMISHA.. ATOA SIKU 14


Dokta Manyaunyau ambae ameombwa kuwa wa kwanza kujisalimisha kwake
kutokana na matatizo makubwa aliyokuwa nayo.

Na Mwandishi wa Maskanibongotz
Katika hali isiyokuwa ya kawaida Nabii Jerry wa kanisa la Holly Ghost Fire lilipo Mbezi Juu kwa Temba Jijini Dar ametoa mpya baada ya kuwatangazia kiama waganga wote wanaotumika kwa ushirikina pamoja na wachawi kujisalimisha kanisani kwake mara moja kabla moto wake haujatua kwenye vichwa vyao.
Akiongea na waandishi wa habari mbalimbali Kanisani kwake mwishoni mwa juma Nabii huyo alisema kuwa katika maono yake amegundua jinsi gani waganga wa kienyeji baadhi na wachawi  jinsi wanavyoaathiri maisha ya wakazi wa Jiji.
Nabii Jerry aliongeza kusema" Natamka hadharani mbele ya vyombo vya habari juu ya hawa waganga wakienyeji na wachawi nawatangazia vita juu yao na natoa siku 14 wawe wamejisalimisha mahara hapa kwa ajili kuchoma hizo tungur zao na endapo watakiuka maagizo haya basi moto wa injiili utawafanya vibaya na kuumbuka kwenye jamii" Alisema Nabii Jerry
Mtumishi huyo wa Mungu amekuwa na kalama ya kipekee huku maelfu ya wananchi wakimiminika kanisani kwake kwa ajili ya kupata msaada wa haraka, na amekuwa kati na manabii tofauti kwenye kutoa huduma ya maombi nchini kwani yeyey humuombe mtu na kuponywa ugonjwa wake papo hapo na sio longolongo.


Aidha nae Mtumishi huyo hakusita kutoa uwito kwa wakazi wote wa Jiji la Dar kuendelea kumiminika kwenye Huduma yake kwa ajili ya kazi moja tu ya Uponyaji na maombi maalum na hii ndiyo namba yake ya huduma kwa maombi +225713-976786 Na ratiba zinaanza kila siku za Jumatano, Alhamisi, Ijumaa, Jumamosi, ni saa kumi jino  na Jumapili ibada inaanza saa tatu asubuhi hasi saa saba mchana. 
Na tayari maamia ya watu wamefungulia maradhi yao hadi sasa wako huru kila hitaji kwake linafanikiwa kwa kipindi kifupi na huo ndiyo moto unavyofanyakazi kwa Mchungaji huyo.

0 comments:

Post a Comment