MKURUGENZI wa
bendi ya Extra Bongo, Ali Choki amepata pigo la kuondokewa na mke wake,
Shuea Hamis ‘Mama Shuu’ baada ya kuugua kwa muda mrefu Usiku wa kuamkia
leo.
Akizungumza kwa masikitiko Ali Choki alisema mke wake ameugua kwa muda
wa miezi tisa akiwa anasumbuliwa na mguu ambapo alitibiwa nchini India
ikashindikana akarudishwa nyumbani mpaka mauti yalipomfika usiku wa
kuamkia Jumamosi iliyopita.
“Ukweli nimeumia kwani mke wangu ndiye aliyekuwa mshauri wangu mkuu na
ndiye kila kitu kwangu alikuwa akinisapoti kwenye kazi yangu ya muziki
lakini ndiyo hivyo Mungu amempenda zaidi sina la kufanya,”alisema Ali
Choki.
Aidha Choki alisema mipango ya mazishi ilifanyika nyumbani kwao Tuangoma
Kigamboni na mazishi ya mkewe yatafanyika siku ya kesho saa kumi jioni
katika makaburi ya Chang’ombe Madukamawili.
0 comments:
Post a Comment