Saturday, 25 October 2014

DARASA LA MAPENZI:HIVI KWANINI UMNYIME MPENZI WAKO TUNDA LA CHUMBANI??



ASALAAM aleikhumu/Bwana Yesu asifiwe!

Leo wanawake wenzangu kwenye safu yetu hii pendwa nimewaletea mada moja nzito ambayo ukiiendekeza unavunja nyumba yako hivihivi unajiona.

Hata kama kuna kisa kilichosababisha mgombane, usiruhusu hali hiyo itokee, mwanamke mwenzangu fahamu ugomvi ndani ya nyumba ni mgeni wa kuingia na kutoka, ni shetani huyu, usimruhusu kwako.
Pia elewa mwanamke mwenzangu kuwa ndoa ni kifundo cha mua, unapoutafuna unakuwa mtamu, ikiwa wakati ule unapoutafuna na kuusikia kuwa ni mtamu ndiyo wakati wa raha na starehe katika ndoa.

‘Bata’ zote unazokutana nazo siku za mwanzo wa ndoa yako zinatakiwa kuendelezwa siku zote, mtaambiana tukale bata huku au kule.
Mnaweza kujikuta mnasema leo twende hotelini na mahaba yetu tukamalizie huko,  huo ndiyo wakati wa mua mtamu lakini kuna siku utakutana na fundo kubwa katika mua na siku hiyo utabaini mgeni katika ndoa yenu na si mwingine ni ugomvi.

Mgeni huyo ni kama fundo la mua. Ikiwa wewe utaruhusu huo ugomvi uendelee kwa muda wa mwezi, je ndiyo utamnyima mumeo unyumba kwa siku zote hizo?
Dini zote mbili kunyimana unyumba ni dhambi. Lakini hata kisheria ni kosa kubwa sana. Je, unataka mumeo aende wapi? akapate burudani kama atakayopata kwako wewe mkewe kwa nani?

Kama mwezi mzima wewe utakuwa ‘unamchunia’ eti kwa sababu amekuudhi na hutaki kurudisha mapenzi na kumsamehe mumeo kosa linalosameheka unadhani atafanya nini?
 Kumbuka kuwa hakuna kosa lisilosameheka kwenye ndoa na ulishakula kiapo kanisani au kwa shehe kwamba mtavumiliana kwa shida na raha. Vitabu vitakatifu pia vinasema msamehe aliyekukosea saba mara sabini!    


Wanawake wenzangu mpo wengi wenye tabia hizo, mwanaume akikukosea kidogo tu fimbo ndiyo hilo la kumnyima unyumba. Ndoa tamu bibi, asikwambie mtu. Watu wanakesha wakizitafuta ndoa kwa waganga, makanisani na misikitini. Wengine hospitali kwa kusafisha vizazi, wewe umepata halafu unaichezea? Acha hizo.
Leo mumeo unampa adhabu hiyo, atabebwa juu kwa juu huyo! Atakwenda kutafuta burudani nje utapata faida gani? Halooooo shauri yako, utakuja kuchekwa Heheeeeee, utalijua jiji!

0 comments:

Post a Comment