MAPENZI yamegeuka shubiri, usaliti na maumivu ya moyo yamegeuka na kuwa
sehemu ya kawaida katika uhusiano wa kimapenzi. Zaidi ya asilimia 50 ya wanandoa, wanalia kuwa wanasalitiwa au waliwahi kusalitiwa na wenzi wao, si wanawake, si wanaume.
Zipo
sababu nyingi zinazosababisha usaliti lakini lengo langu leo siyo
kuzungumzia hilo bali ni kujaribu kuiponya mioyo ya wanandoa au watu
wanaoishi kwenye uhusiano wa kimapenzi, waliojeruhiwa na usaliti.
Yawezekana ulitokea kumpenda sana mwenzi wako, ukaamini wewe ndiyo kila kitu kwake, ukamtimizia kila kilichokuwa ndani ya uwezo wako lakini mwisho, ukaambulia maumivu baada ya kugundua kuwa yupo mwingine anayekuibia mali zako.
Yawezekana ulitokea kumpenda sana mwenzi wako, ukaamini wewe ndiyo kila kitu kwake, ukamtimizia kila kilichokuwa ndani ya uwezo wako lakini mwisho, ukaambulia maumivu baada ya kugundua kuwa yupo mwingine anayekuibia mali zako.
Tujenge
hoja! Vitabu vya dini mbalimbali vinaeleza kuwa kosa pekee linaloweza
kuivunja ndoa, hata ile iliyofungwa kwa baraka za Mungu, iwe ni
madhabahuni au msikitini, ni USALITI.
Sitaki
kupingana na maandiko hayo lakini nataka tujadiliane, ni lazima kila
unapogundua kuwa mwenzi wako amekusaliti dawa yake ni kupeana talaka au
kuachana kwa ugomvi? Dunia imebadilika, wanaume wengi wanasaliti ndoa
zao kwa sababu moja au nyingine, hali kadhalika wanawake.
Mathalani
umefunga ndoa na kuishi na mwenzi wako kwa kipindi kirefu mkipendana,
kujaliana na kuoneshana kila aina ya mahaba lakini akateleza na
kukusaliti ilihali bado anakupenda, utakapoamua kuachana naye na kwenda
kwa mwingine, ukigundua naye anakusaliti utafanya nini? Utaachana na
wangapi? Utaolewa na kuachika mara ngapi?
Bila
shaka umeanza kunielewa kwamba siyo mara zote talaka au kuachana ndiyo
suluhisho la usaliti ndani ya ndoa. La hasha! Siwafundishi watu wasaliti
ndoa zao au uhusiano wao kwa makusudi wakitegemea kusamehewa, hapana.
Ninachotaka
kukijengea hoja ni kwamba, hata baada ya mwenzi wako kukusaliti, bado
mna nafasi ya kuendelea na maisha yenu ikiwa tu mtaamua kulishughulikia
tatizo hilo kwa kina bila kujali watu wa nje wanasemaje.
Usikilize
moyo wako, ni kweli amekusaliti! Amekuumiza, unahisi dunia yote
imekuelemea, unatamani kufa au kuua, lakini je, moyo wako unakuambia
nini? Upo tayari kumruhusu mwizi wako ndiyo awe mmiliki halali wa mwenzi
wako ambaye umetumia muda mrefu kumjenga awe vile unavyotaka?
Jibu
sahihi halitapatikana kwa kukurupuka, hakuna uamuzi wa busara unaotoka
ukiwa na hasira, jazba au ukiwa na shinikizo kubwa kutoka kwa marafiki,
ndugu, majirani na watu wanaokuzunguka.
Pata muda wa kurelax kisha usikilize moyo wako, majibu yatakayotoka ukiwa umetulia, ndiyo yatakayoamua kama uendelee au usiendelee na uhusiano uliosababisha ukaumia.
Pata muda wa kurelax kisha usikilize moyo wako, majibu yatakayotoka ukiwa umetulia, ndiyo yatakayoamua kama uendelee au usiendelee na uhusiano uliosababisha ukaumia.
Yawezekana
wewe ndiyo ulikuwa sababu ya mwenzako kuchepuka, au ni tamaa za kimwili
ndizo zilizomsukuma kuyafanya hayo, lakini jambo la msingi ni
kujiuliza; bado anakupenda? Anaonesha kujutia makosa yake? Anakiri na
kukuomba msamaha? Kabla hajakusaliti, mmefanya mambo mangapi mazuri?
Tuliza akili kisha amua.
0 comments:
Post a Comment