Friday, 3 October 2014

EXCLUSIVE: SOMA MANENO MAZITO YA T.I.D MNYAMA .




MKONGWE wa muziki wa kizazi kipya nchini, Khalid Mohammed ‘TID
Mnyama’ amesema, yeye ni msanii wa kimataifa tangu siku nyingi ingawa amekuwa hapewi sapoti anayostahili kupata.
Akizunguza jijini Dar es Salaam, muimbaji huyo ambaye hivi karibuni alirekodi wimbo na msanii wa Afrika Kusini, Tumi, amesema kile wanachokifanya wasanii wapya wanaotaka kwenda kimataifa kwa sasa, yeye alikifanya miaka mingi iliyopita.
Unajua kama kufanya muziki kimataifa mimi tayari nilishaenda zamani sana, maana nikikumbuka video zangu nimeshafanya mahojiano na MTV Base, Channel O na pia nimefanya kazi na wasanii kutoka Nigeria na Afrika Kusini

alisema TID.
Pia nimefanya kazi na watu kama akina Dk Chameleone na wasanii wengine, kwa hiyo kwenda kimataifa ndo kitu nachokifanya. Naona ni sapoti tu ndio siipati ya kutosha maana nimeshafanya matamasha makubwa kama Rwanda, Burundi na Afrika Kusini, kwa hiyo muziki wangu upo kimataifa
alisema.
TID aliwahi kutamba na albamu zake mbili za Zeze na ‘Nyota Yangu’ zilizofanya vizuri na kumtangaza katika nchi za jira

0 comments:

Post a Comment