MAJERUHI 9
kati ya 15 waliofikishwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya
kuungua na moto uliosababishwa na kuungua kwa lori la mafuta huko
Mbagala jijini Dar es Salaam Oktoba 15 mwaka huu, wanaendelea na
matibabu huku hali zao zikiwa bado mbaya.
Kamera yetu ilifika katika hospitali hiyo na kuwakuta wagonjwa hao
wakiwa wamelazwa katika wodi namba 23 iliyopo katika jengo la Sewahaji
na Afisa Uhusiano msaidizi wa Muhimbili, Doris Ihenga alisema majeruhi
sita waliokuja pamoja nao, wamefariki dunia.
Alisema majeruhi wawili kati ya tisa waliolazwa, hali zao ni mbaya zaidi
ambao aliwataja majina yao kuwa ni Mathayo Danie (21) na Hamis Ally
(35).
Wengine waliolazwa kwa kuunguzwa na moto huo wakati wakijaribu kuchota
mafuta yaliyomwagika kutoka kwenye tenki la gari lililoanguka ni Abbas
Mohamed (25), Hamis Kambi (25) Idd Said (30) Mathayo Daniel (21) Hamis
Ally (35) Ibrahimu Hamis (26) Maganga Mgombele (38) na Shabaki Martin.
0 comments:
Post a Comment