Tuesday, 4 November 2014

JE WAJUA KILICHOMRUDISHA RIHANA INSTAGRAM, SOMA HAPA




Kimya cha miezi sita huenda kikarudi na mengi kumhusu mkali Robyn Rihanna
Fenty a.k.a Rihanna, ambaye imeripotiwa kuwa amerudi tena katika mtandao wa Instagram kuungana na fans wake zaidi ya milioni 12 baada ya kuwatelekeza kwa kipindi cha miezi 6 ambapo picha ya mwisho kuiweka katika akaunti yake ilikuwa Mei 3 mwaka huu.
Tangu arudi saa 24 zilizopita tayari ame post picha 11 kwenye ukurasa wake.
Rafiki wa karibu wa Rihanna mwanamitindo Tom Ford amesema kujitoa kwa msanii huyo Instagram ilikuwa hasara kubwa kwa kupoteza wapenzi biashara yake ya fashion, hivyo kurudi kwake kutasaidia kuiokoa hasara hiyo kwa kiasi kikubwa.


Instagram wamemkaribisha Rihanna kwa mikono miwili kupitia ukurasa wao wa 


Twitter kwa kuandika, “Welcome back @rihanna! #RIHunited #badgalback”– Instagram

0 comments:

Post a Comment