Wednesday, 3 December 2014

DARASA LA MAPENZI..!! CHUMA CHA MOTO HAKIZIMWI KWA MAJI BARIDI!

Nami vilevile kwa nini niwanyime uhondo kitu ambacho nimekipata katika raha zangu? Shoga huu ni unyago wa bure, japo si kungwi kihivyo, lakini kaa chini nikufunde ufundike, sipendi kutiwa aibu na mwanamke mwenzangu, aibu hivyo mbayaaaa eeeh?


Mmh! Yaani kufungua gazeti tu umeanza na mimi, inaonekana ulikuwa
ukinisubiri kwa hamu kubwa, nipo nimejaa tele kama pishi la mchele. Kuna baadhi ya makabila husema kwa nini akunyime kitu ambacho amekikuta mwilini mwake.
Leo mwakwetu nimerudi ndani ya nyumba baada ya kukupendeleeni shangingi mnaofuata nyayo zangu. Kutokana na maombi ya wanawake wengi walio ndani ya ndoa kuomba nao niwape upendeleo ili wadumu kwenye ndoa zao. Nami kama nilivyosema ni mtu wenu, nitumieni mtakavyo kwa vile bado nina pumzi pia nina uwezo wa kusema ninachokijua kwa ufasaha zaidi pengine kuliko aliye katika ndoa.
Kuna kitu kimoja kimenikera kutoka kwa wanawake wenzangu kwa kutoelewa eneo lipi afanye kipi na eneo lipi asifanye. Pamoja na kuwa mzungumzaji wao mkuu, nimekuwa nikipokea matatizo ya uhusiano toka kwa wanaume. Mwanaume mmoja alijiuliza eti ni sawa mkeo kuanza kutoa lawama mkiwa kitandani tena kipindi hicho mnaanzisha muziki, mwenzako anajiandaa kucheza wewe unazima muziki na kuanza kufungua matatizo yako.

Najua wewe huamini unamkomoa, kwamba ukizima muziki matatizo yako yatasikilizwa. Lakini siyo, sehemu ya starehe ifanyike starehe na sehemu ya malalamiko yawe malalamiko. Huwezi kumpandisha mtu mzuka kisha unasimamisha bila sababu ya msingi, kisa eti utasikilizwa.
Ni sawa na kukizima chuma kwa maji baridi lazima kitapinda, hali kadhalika katika starehe za kitandani. Nataka leo nikupeni njia ya kuomba au kutoa lawama zako kwa mumeo au mpenzio bila kumuudhi. Sipendi kuelezea kwa maneno bali vitendo ili ujue kila nikisemacho nilikifanyia kazi.
Siku moja buzi langu ambalo lilikuwa pamanent lazima nilale kwake ambalo lilidata naweza kusema ndilo lililomalizia nyumba hii japo yupo mwingine naye aliingiza mkono wake, ambaye stori zake ntakupeni siku nyingine.
Basi katika kurushana roho kuna siku nilimuomba anisaidie kumaliza nyumba yangu, hakunikatalia lakini ndiyo ilikuwa kesho kila siku kesho. Mtoto wa kike nilijikuta nikichanganyikiwa, penzi nampa kadri ya uwezo wangu lakini bado aliendelea kunidanganya.
Nilijiuliza nitafanya nini ili anitimizie nilichomuomba kwa vile sikuwa namdai pesa za makubaliano yetu alinipa kama kawaida hata kuzidi kiwango.
Lakini tatizo likabakia kupewa kikubwa ambacho ndicho cha muhimu. Mtoto wa kike mbinu zote nilitumia nijuazo bila mafanikio.

Nami bila aibu nilimfuata bibi yangu kizaa mama na kumuuliza kitu gani aliomfanyia babu kumfanya asioe wanawake wengi tofauti na wazee wengi wa zamani walikuwa wakishindana kuoa. Bibi hakuwa mchoyo alinieleza nami nilikuja kuifanyia kazi.
Ni mimi anti Nasra Shangingi Mstaafu

0 comments:

Post a Comment